Chai FM

Mwenge kuzindua miradi ya zaidi ya shilingi bilioni 15 Rungwe

24 August 2024, 12:48 pm

Miradi mbamlibali inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Wananchi wilayani Rungwe mkoani  Mbeya wameombwa kujitokeza kupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kungia siku ya tarehe 27 mwezi  huu  na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake amesema zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni kumi na tano kimetumika kuaajili ya ujenzi wa miradi

Mkuu wa wilaya ameitaja miradi itakayotembelewa na kukaguliwa nipamoja na stendi mpya ya mabasi iliyopo Tukuyu mjini,Barabara Ntulilo -itete inayojengwa kwa kiwango cha rami,sambamba na bweni la shule ya wavulana Rungwe

sauti ya nkuu wa wilaya 1

Aidha Hanniu amesema mbio za menge wa uhuru zitakimbizwa umali wa  kilometa 80.6 kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kata ya isongole,ndando ,kiwira na maeneo mengine

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Sambamba na hilo mkuu huyo wa wilaya ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara wote kupeleka bidhaa zao kwenye uwanja wa tandale ambapo mwenye wa uhuru utakesha hapo na siku ya tarehe 28 ataukabidhi wilaya ya Kyela

sauti ya mkuu wa wilaya 3