Chai FM

Ajinyonga baada ya gari yake kupata ajali

20 August 2024, 9:47 am

Wivu wa mapenzi na tatizo la uchumi imetajwa kuwa chanzo cha watu wengi kufanya mamuzi magumu hata kuondoa uhai wao wenyewe

Na Sabina Martin – Rungwe

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Shafki Mkwama amekutwa amejingonga nyumbani kwake kijiji cha Ikapu kata ya Kambasegera halmashauri ya wilaya Busokelo wilayani Rungwe huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Chai FM radio imezungumza kwa njia ya simu na diwani wa Kata ya Kambasegera Bw. Abraham Jecob Mwakapimba ameeleza kutokea kwa tukio hilo huku akitoa rai kwa viongozi wa dini, machifu na jamii kila mmoja kwa imani yake kukemea vitendo vya watu kufanya maamuzi magumu ikiwemo kujiua.

Sauti ya diwani kambasegera

Mary Edwin Silulele ni mwenyekiti wa kijiji cha Ikapu ameeleza kwamba baada ya kupewa taarifa na wananchi juu ya uwepo wa tukio hilo wamewasiliana na jeshi la polisi kwaajili ya taratibu zaidi huku akitoa rai kwa jamii kushirikisha wapendwa wao matatizo yanayo wakabili.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji

Baadhi ya majirani wa kijana huyo aliyejinyonga aliyeahamika kwa jina la Shafki Mkwama wamesema kwamba waliishi na kijana huyo kwa upendo kwani alikua akishirikiana na wenzie kwa upendo.

Sauti za majirani

Tukio hilo ni la kwanza kutokea katika eneo la Ikapu kata ya Kambasegera huku baadhi ya wananchi wakihusisha tukio hilo na ajali aliyoipata marehemu hivi karibuni, taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea kwao mkoani Iringa kwaajili ya kumpumzisha zinaendelea.