Chai FM

Baraza la madiwani laazimia kuwafuta kazi watumishi Rungwe

6 August 2024, 11:56 am

Mkuu wa wilaya ya RungweJaffar Hanniu akitoa salamu za serikali kwenye kikao cha Baraza la madiwani[picha na Lennox Mwamakula]

Watumishi wa uma wametakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maadili ya kazi kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Kufuatia halmashauri ya wilaya ya Rungwe kukusanya asilimia 102 ya makusayo ya fedha kwa mapato ya ndani Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh, Jaffar Hanniu  amewapongeza madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji kwa ukusanyaji  wa fedha hizo.

Mkuu huyo wa wilaya  ametoa pongezi hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne ya mwaka kilichokilichofanyika kwenye ukumbi wa John Mwankenja amesema licha ya pongezi hizo  bado kuna upotevu wa fedha hivyo amewataka madiwani kuendelea kumpa ushirikiano mkurugenzi mtendaji wa namna ya kudhibiti minya ya upotevu wa mapato ili kufikia malengo ya kuwa hudumia wananchi

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza[picha na Lennox Mwamakula

sauti ya mkuu wa wilaya 1

Hata hivyo Hanniu ametumia nafasi hiyo ya kuwakumbusha madiwani  kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili ifikapo tarehe ya kuchaguzi waweze kuwachagua viongozi wanaowata na pia amekemea  na kuulani vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemalu wa ngozi [albino] vinavyo jitokeza baadhi ya maeneo nchini.

sauti ya mkuu wa wilaya 2

Aidha kwenye kikao hicho cha baraza la madiwani limeadhimia kuwafuta kazi watumishi wawili wa umma muuguzi wa afya pamoja na afisa mtendaji wa kijiji  Ndg, Daniel Langeni kwa kutofika kazini kwa muda mrefu bila kuto taarifa hivyo baraza

sauti ya mwenyekiti wa halmashauri

Pia mkuu huyo wa wilaya amewaomba watalaamu kusimamia maamuzi ya madiwani kwani kikao cha Baraza ndicho kikao halali cha namna kupanga mikakati ya maendeleo ndani ya halmashauri kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo

sauti ya mkuu wa wilaya 3

Sambamba  na hilo mkuu wa wilaya ya Rungwe ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tazania  Dr, Samia Suluhu Hassan kwakuipatia wilaya ya Rungwe fendha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwemo miradi  ya maji,umeme ujenzi wa vyumba vya madarasa ,vituo vya afya pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya  Barabara