Chai FM

Zaidi ya shilingi bilioni 2.9 kujenga kituo jumuishi Rungwe

4 August 2024, 3:10 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Renatus Mchau akizungumza kwenye makabidhino y mradi [Picha na Lennox Mwamakula]

Zao la parachichi linakwenda kuongezewa thamani baada ya serilikali kujenga kituo cha kuhifadhia mbogamboga na matunda.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa kituo jumuishi cha kuongeza thamani ya mazao ya bustani hususani parachichi amekabidhiwa eneo la utekelezaji wa mradi huu lililopo kijiji cha Nkunga kata ya Nkunga.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Renatus Mchau amesema kumekuwepo kwa changamoto mbalimbali za zao la parachichi hivyo changamto hizo zinakwenda kutatuliwa na kuwaomba wananchi kutumia fursa iliyojitokeza kwenye eneo hilo la mradi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa akizungumza kwenye hafla ya kumkabidhi mkandarasi [picha na lennox mwamakula]
Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo Ndg, Frolian Kalemela amesema ujenzi wa kituo kicho unaenda kumaliza changamoto za wakulima pia utaongeza ubora wa mazao kwa ujumla.

Sauti ya mwakilishi wa Wizara ya Kilimo

Kituo hiki kitakuwa na uwezo wa kukusanya, kuchambua, kupanga madaraja na kuhifadhi mazao kama parachichi.

Naye mwakilishi wa mkandarasi wa kampuni  ya Skyward Construction itakayojenga kituo hicho amewatoa hofu wananchi kuwa mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa.

Sauti ya Mwakatobe

Sambamba na hilo kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa amewaomba wakazi wa eneo hilo kuwa walinzi na kumpa ushirikiano mkandarasi anayetekeleza mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

Sauti ya Katibu Tawala

Zaidi ya shilingi bilioni 2.9 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huu; fedha iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Kilimo.