Chai FM

Baraza la madiwani lakemea vitendo vya ulawiti Busokelo

4 August 2024, 1:26 pm

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jafarr Hanniu akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Busokeo Bi, Loema Peter [Picha na Lennox Mwamakula]

Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ukatili jamii imetakiwa kutoa taarifa kwa vingozi wa serikali ili kuweza kuwabaini watu wanaofanya vitendo hivyo.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya  sheria baada ya kuwabaini watu wenye tabia ya kuwaficha watuhumiwa wa makosa ya vitendo vya ulawiti kwa watoto maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu wakati wa kikao cha nne cha robo  mwaka cha Baraza la Madiwani halmashauri ya Busokelo baada ya diwani wa kata ya Isange Elias Mwasendele kueleza ongezeko la  vitendo vya ulawiti unaofanywa na baadhi ya wananchi huku afisa ustawi wa jamii akitoa takwimu za vitendo hivyo katika halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Busokelo akikabidhiwa cheti na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe [Picha na Lennox Mwamakula]
Sauti Elias Mwasendele Diwani kata ya Isange

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Busokelo Anyosisye Njobelo amewataka madiwani pamoja na jamii kulaani vitendo vya ulawiti vinavyoendelea  kushamiri katika kata zao.

Sauti ya Anyosisye Njobelo Mwenyekiti Baraza la Madiwani Halmashauri ya Busokelo

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amesema kesi za ulawiti zinakosa ushahidi baada ya mashahidi kutokutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria jambo linalosababisha watuhumiwa kutochukuliwa hatua.

Sauti ya DC Haniu

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewatunuku vyeti mwenyekiti wa halmashauri ya Busokelo pamoja na mkurugenzi mtendaji kwa ushirikiano mzuri walionao wa ukusanyaji wa mapato na usimamiaji wa miradi inayotekelezwa ndani ya halmashauri hiyo.

Sauti ya DC Haniu

Kwa upande wao madiwani wamemshukuru mkuu wa wilaya ya Rungwe kwa kuthamini mchango wao wa utendaji wa kazi na wamesema amekuwa mkuu wa wilaya wa kwanza kutambua kazi yao.

Sauti ya diwani