Elimu kutolewa juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto Busokelo
30 July 2024, 3:47 pm
ASP Mstapher akitoa kwa wananchielimu juu ya vitendo ukatili
ili kukabiliana na vitendo ya ukatili kwenye jamii jeshi la polisi limeomba ushirikiano ili kuwabaini wanao fanya vitendo hivyo.
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox mwamakula
Jamii imeshauriwa kutoa ushirkiano kwenye jeshi la polisi pindi jeshi hilo linapo fanya uchunguzi wa jambo lolote lililo kuwa na viashilia vya uvunjjifu wa amani
Kauli hiyo imetelewa na mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi kituo cha polisi lwangwa kilichopo halmashauri ya Busokelo alipokuwa akitoa elimu juu vya vitendo vya ukatili vinavyo endelea kutokea kwenye jamii
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya busokelo Bi, loema peter akiwaomba wazazi na walezi kuwa karibu na watoto kutokana na vitendo vya ukatili
Elimu hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika lwangwa mjini wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la busokelo ya kijiji kwa kijiji ya kusikilza kero za wananchi ambapo mmoja ya wananchi aliwasilisha kero ya kuwa anashangazwa kusikia matukio kuwa vijana wa kiume wanaoana wenyewe kwa wenyewe na kusema kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria
sauti ya mwananchi
Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya busokelo Bi, Loema peter amesema kwenye jamii kuna wimbi kubwa la unyanyasaji wa kijinsia watoto wanafanyiwa vitendo vya ukatili ikiwa ni kulawitiwa,hivyo amewaomba wazazi kuwa makini na watoto
sauti ya mkurugenzi
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi lwangwa ASP Mstapher amesema wao kama jeshi la polisi wanapata taarifa za kuwapo kwa vitendo hivyo na wanawachukulia hatua wale wote wanaofanya vitendo hivyo na kuwaomba wazazi wawe na utaratibu wa kuwaogesha watoto na kuwakagua
sauti ya ASP mstapher 1
Hata hivyo ASP Mstapher baadhi ya wazazi wamekuwa na utaratibu ya kutotoa taarifa kwenye vyombo vya kisheria na kumalizana kienyeji hiyo ameomba jamii kutoa ushirikiano pindi watu wanapo fanya vitendo hivyo visivyo kubarika kwenye jamii
sauti ya ASP mstapher 2