Chai FM

Wananchi waomba afisa mtendaji kuchunguzwa Busokelo

28 July 2024, 11:47 am

kutokana na kuwamaa kwa ujenzi wa zahanati wananchi wametoa malalamiko yao mbele ya mbunge ili aweze kuwaondolea mtendaji wa kijiji

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox mwamakula

Wananchi wa kijiji cha lulasi kata ya Mpombo halmashauri ya busokelo wameviomba vyombo vya uchunguzi kumchunguza mtendaji wa kijiji juu ya mali za umma

Kauli wameitoa mbele ya mbunge wa jimbo la Busokelo mh,  Atupele mwakibete kwenye ziara ya kusikiliza kero za wananchi ya kijiji kwa kijiji anayoifanya jimboni humo

Mbunge huyo akiwa katika katika kijiji cha lulasi wananchi wamewasilisha kero zao mbalimbali ikiwemo suala la mpotevu wa mbao za kijiji pamoja na tofari kwa madai ya kuwa ametumia kwa matumizi yake binafsi

sauti za wananchi

Naye Neema Mwaipopo mkazi wa kijiji hicho cha lulasi wa amesema ni takribani miaka kumi na mitano ujenzi wa zahanati umekwama na wanashindwa kupata huduma

sauti za wananchi zahanati

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho cha lulasi amesema anashangazwa na taarifa za malalamiko zinazo tolewa na wanachi hao kwani taarifa za mapato na matumizi zinazomwa  kwa mujibu wa sheria

sauti ya afisa mtendaji

Aidha Mh,mbunge  Mwakibete amesema suala la mtendaji wa kijiji amelichukua na linaenda kufanyiwa kazi ili wananchi hao waendelea kuwa na imani na watumishi wao

sauti ya mbunge