Chai FM

Kuelekea msimu mpya wa NBC Premier League wadau watoa ya moyoni

26 July 2024, 1:12 pm

Wakati vilabu mbalimbali vya mpira vinavyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC vikijiandaa na msimu mpya wa ligi mashabiki wa mpira wamekuwa na maoni tofauti kulingana na sajili zilizofanywa na vilabu vyao.

Na Gwamaka Mwakisyala – Rungwe

Kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya NBC Premier League wadau wa soka wilayani Rungwe wameeleza hisi zao kutokana sajili zilizofanywa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi kuu.

Felix Aden, Shedrack Ally na Brown ni miongoni mwa wadau wa michezo wilayani hapa wameeleza kwamba huenda Yanga akatwaa ubingwa kulingana na usajili walioufanya huku wakieleza ushindani mkubwa unatarajiwa katika msimu huu.

sauti za mashabiki wa mpira wilayani Rungwe

Kwa upande mwingine mdau wa soka hapa wilayani Rungwe Gega Lee amesifu usajili wa klabu ya Yanga kuwa umelenga mashindano ya kimataifa huku akiwamwagia sifa Duke Abuya, Aziz Andambwile, Maxi Mpia Nzengeli pamoja na Clatus Chota Chama.

Sauti ya mdau wa mpira Gega

Mwenyekiti wa tawi la Yanga Tukuyu mjini Ndg. Meswin Mdala Ndunguru amekiri kuendelea na ubabe kuelekea msimu ujao kutokana na ongezeko la wachezaji sita katika kikosi hicho, huku akitoa dongo kwa wapinzani wao kuwa wataendeleza kuwashushia kichapo cha goli tano msimu ujao.

Sauti ya mwenyekiti tawi la Yanga Tukuyu