Chai FM

Mbunge akemea tabia za wizi wa nguzo za umeme jimbo la Busokelo

14 July 2024, 12:22 pm

Mbunge wa jimbo la Busokelo akiongea na wananchi

Kuwepo kwa watumishi wa umma wasio waaminifu kunapelekea kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

BUSOKELO-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Freddy Mwakibete amemwagiza Meneja wa Tanesco wa halmashauri ya Busokelo kuzirejesha nguzo za umeme zilizoibwa kwenye makazi na wananchi na kukosa huduma ya umeme kwa muda mrefu.

Ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya mbunge hiyo anayoifanya ya kusikiliza kero za wananchi ya kijiji kwa kijiji alipokuwa kijiji cha Mpanda kata ya Lupata baada ya wananchi hao kuwasilisha changamoto zinazowakabili.

Wananchi wa kijiji hicho cha Mpanda wamesema wameshwangazwa na vitendo vya watumishi wa shirika hilo la umeme nchini kutokana na tabia iliyoibuka ndani ya kata yao ya kuibiwa nguzo za umeme zilizopelekwa kijijini hapo ili wananchi wapate umeme kuna watu huingia kijijini hapo na kuziiba nguzo hizo kitendo kinanchowasikitisha wananchi hao.

Wananchi wakimpokea Mbunge wao
Sauti za wananchi wakitoa kero mbele ya Mbunge

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Tanesco halmashauri ya Busokelo amekiri kuwepo kwa taarifa hizo ofisini kwao na amesema wamewachukilia hatua za kisheria wote waliofanya kitendo hicho.

Sauti ya Kaimu Meneja Tanesco

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Busokelo Mh, Anyosisye Mjobelo amesema Tanesco wazirudishe nguzo hizo maeneo husika kwani kitendo kinachofanywa na baadhi ya watumishi wasio waminifu hakikubaliki kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya watu pamoja na kukwamisha jitihada zinazofanywa na serikali.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri….

Aidha Mbunge wa Jimbo hilo Mh, Atupele Mwakibete amesikitishwa na vitendo hivyo vya kuwahujumu wananchi kwenye miundombonu kwani serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Amesema kitendo hicho hakikubaliki wale wote waliohusika na wizi huo wachukuliwe hatua za kisheria.

Sauti ya mbunge

Mh, Mwakibete amewaomba wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwani  ipo kwa ajili ya kuwatumikia.