Vitendo vya ukatili kwa watoto kukomeshwa Rungwe
16 June 2024, 8:45 pm
wadau wa kupinga vitendo vya ukatili kushirikiana na wazazi kutokomeza vitendo vya vya ukatili vilivyopo kwenye maeneo mbalimbali wilayani Rungwe
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Ikiwa kila ifikapo juni 16 Tanzania inaungana na mataifa mengine ya nchi za Afrika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa dhumuni la kumlinda mtoto na vitendo vya ukatili anavyo weza kutendewa kwenye jamii
wadau na wanafunzi walioshiriki kwenye maadhimisho ya mtoto wa afrika
Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe aliye wakilishwa na Katibu tawala wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Ndg Ally Kiumwa amemwangiza mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Rungwe kufanya majadiliano upya ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyoendelea kuripotiwa licha ya kuwapo kwa mashirika yanayo tekeleza miradi ya kupinga ukatili dhidi ya watoto
katibu tawala ndg Ally kiumwa akizungumza siku ya maadhimisho ya mtoto wa afrika[picha na Lennox Mwamakula]
Kiumwa ametoa kauli hiyo kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi katumba II Iliyopo kata ya ibighi wilaya Rungwe ambapo amesema kuna haja ya jamii kuungana kupinga vitendo hivyo na kutoa taarifa kwa viongozi wa maeneo yetu wakiwemo wenyevit wa mitaa /vijiji na kwenye maadawati ya kutetea haki za mtoto
Mmoja ya wanafunzi akisoma risala mbele ya mgeni rasmi[ picha na lennox Mwamakula]
sauti ya kiumwa 1
Akisoma Risala mmoja ya wanafunzi wa shule ya msingi katumba II wanafunzi wamebainisha changamoto zinazowakabili kwaani wamesema lisha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya ukatili, bado vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaendelea kama vile kubakwa,kurawitiwa ,mimba za utotoni na kukosa mirathi pindi wazazi wao wakifariki
sauti ya risala 1
Hata hivyo wanafunzi hao wameioma serikali kuwajengea miundombinu rafiki ya kufundishiwa ili kuwawezesha kupata elimu jumuishi na kuweka mazingira rafiki
sauti ya risala 2
Akijibu risala hiyo katibu tawala wa wilaya ya Rungwe Ally Kiumwa amewaomba wazazi kuto wafisha watoto wenye ulemavu kwani amesema hata wao wana haki ya kupata mahitaji yote ya msingi ikiwa ni pamoja na elimu hivyo jamii ijenge tamaduni ya kuwapeleka watoto waote shule ili waweze kupata haki zao za msingi
sauti ya kiumwa 2
Kwa upande wake afisa miradi kutoa shirika la Dsw Tanzania amesema watandelea kushirikiana na serikali kukabiliana na kupinga vitendo vya ukatili na amewaomba wana Rungwe kutoa ushirikiano kwa wadau waliopo kwenye maeneo yao
sauti ya afisa mradi 1
Ikumbukwe kuwa chimbuko la maadhimisho ya mtoto wa afrika ni Azimio lililopitishwa na ulikuwa nai umoja wa Nchi huru za kiafrika [OAU] Mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini afrika kusini waliouwawa tarehe 16 Juni,mwaka 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi.