Mkandarasi apewa wiki tatu kukamilisha stendi Rungwe
4 June 2024, 5:14 pm
Ili kuboresha miundombinu wananchi wametakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa serikali pindi inapotekelezwa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh, Juma Homera amemwagiza mkandarasi anayejenga stendi ya Mabasi Tukuyu kuikamilisha ndani ya wiki tatu ili iweze kuanza kutumika
Homera ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo ya mabasiinayo jengwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya Rungwe katika mji mdogo wa tukuyu stendi ambayo imekuwa kilio cha muda mrefu cha wananchi
Mkuu wa koa wa Mbeya mh, Juma Homera akitoa maagizo ya utekelezaji wa stendi ya mabasi Tukuyu
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi mhandisi Eng, Omary Mataka amesema mradi huo umefikia asilimi 77 na pindi utakapo kamilika wananchi pamoja na wafanyabiashara watanufaika baada ya kuwekea mazingira rafiki ya kufanyia shughuli zao za kujingizia kipato
sauti ya mhandasi akisoma taarifa
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu akitoa salamu kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Rungwe amesema wananchi wanamshukuru rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi mbakimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya wilaya ikiwa ni pamoja na mradi ya elimu,afya na maji
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu akitoa pongezi mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa rais Samia kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Rungwe
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu
Akiongea mbele ya wananchi mkuu wa mkoa mh,Homera amesema kumekuwa na kusuasua kwa ujenzi wa stendi hiyo hivyo mkandarasi akishindwa kukamilisha kwa muda aliopewa hatua stahiki sitashukuliwa dhidi yake
wananchi wakiwa stendi ya mabasi tukuyu wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa mbeya alipokuwa akitoa maagizo ya ukamilishaji wa stendi
Sauti ya mkuu wa mkoa Juma Homera 1
Hata hivyo Homera amewaomba wananchi kuachana na tabia ya kulalamika kuwa maisha magumu bali wajishughulishe ka shughuli ndogondogo kwani amesema kutawasadia kujikwamua kiuchumi na amengeza kuwa serikali imeandaa utaratibu wa kutoa fedha za mikopo kwa mwananchi anaye jishughulisha
Sauti ya mkuu wa mkoa Juma Homera 2