Chai FM

Chamata Rungwe imewagusa wazazi

29 May 2024, 3:39 pm

Mganga mkuu wa hospital ya wilaya ya Rungwe akimshukuru mwenyekiti wa chamata [picha na Lennox Mwamakula]

wakazi wa Rungwe wameshauriwa kujenga tabia ya kuwatembelea wagonjwa kwenye hospitali na hata majumbani kwa dhumuni la kufarijiana

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Jamii imetakiwa kuwa na utaratibu wa kuwaona watu wanao kabiliwa na changamoto mbalimbali wakiweno wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya na katika hospitali zote hapa nchini.

Kauli hiyo imetolwea na mwenyekiti wa jumuiya ya chamata wilaya ya Rungwe Bi,Atuganile Samalinga  walipo fanya ziara ya kutembelea hospital ya wilaya ya Rungwe[MAKANDANA] kwenye wadi la mama na mtoto ikiwa ni sehemu ya kuwafariji.

Bi, Atuganile amesema wamefika hospitalini hapo kwa lengo la kuunga jitihada za mweshimiwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwajali watanzania kwa kuwaboreshea huduma ya afya hususani  huduma ya mama na mtoto kwa kila hospital na kwenye vituo vya afya .

Hata hivyo Bi,Atuganile amevitaja vitu ambavyo wamekabidhi kwenye wadi hilo la mama na mtoto kuwa ni sabuni pamoja na taulo za kike

sauti ya Mwenyekiti chamata Rungwe

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe Dr.Declous Ngaiza amewashukuru kwa kufika katika hospitali hiyo na kuwaona wagonjwa wanaoendelea kupatiwa huduma za matibabu na amesema kwa upande wa huduma zinaendelea vizuri

mwekiti wa chamata Rungwe akimkabidhi vifaa mmoja ya wagonjwa [picha na Lennox Mwamakula]

sauti ya DMO

Naye muuguzi kiongozi  wadi la wazazi Emilia Mgaya kwaniaba ya wauguzi amewashukuru jumuiya ya chamata kwakuwaona wakina mama pamoja na watoto waliopo kwenye wadi hilo

Sauti ya muuguzi kiongozi

Aidha nao wakina mama waliolazwa kwenye wadi hilo wamemshukuru rais Samia suluhu Hasani kwa kuwakumbuka  wakina mama wa hali ya chini na kuwapatia vifaa hivyo na wametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakina mamam wote kumuunga mkono kwa jitihada zake

sauti za wakina mama waliolazwa

Sambamba na hilo mwenyekiti wa jumuiya ya chamata wilayani Rungwe amewashukuru wa chama wote waliojitoa kuchangia vitu hivyo kwani amesema wandelee kujitoa kuhudumia jamii ya watu wa Rungwe na Taifa kwa ujumla

sauti ya mwenyekiti neno la shukurani wana chamata