Kakao yawainua wakulima Kyela
14 May 2024, 12:07 pm
Wananchi wa kimsikiliza waziri mkuu kasim majaliwa kwenye viwanja vya AMCOS
Zao la kakao limekuwa mkobozi kwa mkulima kwa miaka ya hivi karibuni.
Na Lennox Mwamakula
Serikali imewapiga marufuku viongozi wa chama kikuu Cha ushirika wilayani kyela mkoani mbeya kwenda kuchukua kokoa za mkulima kwenye vyama vya msingi vilivyopo kwenye vijiji.
Waziri mkuu kasim majaliwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kyela kwenye viwanja vya ofisi za chama kikuu Cha ushirika zilizopo mji ndogo wa ipinda ambapo amesema ili kuimarisha uchumi wa wakulima wa zao la kokoa kila moja wajibike kwa nafasi yake.
shamba la kakao lilipo kata ya mababu lililotembelewa na kwaziri mkuu kasim majaliwa kujionea namna wanavyo zalisha
Sauti ya waziri mkuu
Naye naibu waziri wa viwanda biashara mh,Exaud kigahe amesema baada ya serikali kuweza mfumo wa ununuzi wa zao Hilo Kwa kutumia sitakabadhi ghalani kumesaidia mkulima kuuza kokoa Kwa bei elekezi na kuasha kuwatumia wanunuzi walanguzi maarufu kama mjemke ambayo ununua Kwa bei isiyo mnufaisha mkulima
waziri mkuu akisikiliza maelekezo kwa mkulima wa zao la kokoa namna wanavyo zalisha
sauti ya Naibu waziri wa viwanda na biashara
Aidha wakulima wa zao hilo wamesema zao la kokoa wanakabiliwa na changimoto ya magonjwa mbalimbali ambayo wakulima hawana uwelewa namna ya kuyadhibiti na pia wamesema serikali ijenge kiwanda ndani ya wilaya ya kyela ili waweze kunufaika na zao hilo
sauti za wakulima
Hata hivyo naye david silinde amesema wizara ya viwanda na biashara imeiyagiza taasisi ya utafiti ya kilimo uyole TARI kufanya utafiti wa ugomjwa unao likumba zao la kokoa wilayani kyela
sauti ya David silinde
Ikumbukwe kuwa ziara aliyo ifanya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh, Kasim Majaliwa imelenga kukagua miradi inayotekelezwa maeneo mbalimbali mchini