Elimu ya saratani ya shingo ya kizazi yatolewa Rungwe
9 May 2024, 3:37 pm
Elimu ya afya ya uzazi inatakiwa kuendelea kutolewa kwenye jamii ili kukabiliana na magonjwa yasio ya lazima
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kukabiliana na maradhi mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe Daktari Diocles Ngaiza akitoa elimu kwa njia ya radio juu ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi
Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe dkt Diocles Ngaiza alipokuwa aktoa elimu ya afya juu ya ugonjwa wa shingo ya kizazi kwenye kipindi cha Amka na chai kinacho rushwa na chaifm
Dr Ngaiza amesema sababu zinazo sababisha kuwepo kwa ugonjwa huu,husababishwa na vimelea vinavyo kaa kwenye ngozi ya sehemu ya ume kwa mtu asiye fanyiwa tohara ndiyo maana serikali ilikuja na pango wa Tohara kwa wanaume ikiwa ni sababu moja wapo ya kukabiliana na maradhi kama hayo
sauti ya mganga mkuu wa hospital ya wilaya ya Rungwe 1
Hata amesema ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi inatibika hivyo watu watakiwa kifika kwenye vituo vya afya ili kuweza kuchuzwa tatizo la ugonjwa huo
sauti ya mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe 2
Sambamba na hilo Ngaiza amesema uchunguzi wa Ugonjwa huo wa saratani ya shingo ya kizazi hauna madhara pindi mtu atachunguzwa mapema na kuanza matibabu