Chai FM
Chai FM
13 October 2021, 8:56 am
RUNGWE-MBEYA Wivu wa maendeleo imetajwa kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea waajiri wengi wa wafanyakazi wa majumbani kutowaruhusu wafanyakazi wao kuendesha miradi yao. Wakizungumza na waandishi wetu baadhi ya wananchi wilayani hapa wamesema kwamba baadhi ya waajiri wanaogopa kuzidiwa kipato…
Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.
Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.
Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.
Dira
Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora
Dhamira
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.
Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo
Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa
Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.
Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/