Chai FM
Chai FM
8 November 2021, 6:22 am
RUNGWE-MBEYA Ulaji wa chakula cha mchana katika shule za msingi wilayani Rungwe imechangia kuongeza kiwango cha ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba mwaka huu kutoka asilimia 85.28 ya mwaka jana hadi asilimia 90.59 mwaka huu ambalo ni ongezeko la…
4 November 2021, 4:46 am
RUNGWE Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dr VICENT ANNEY, ameruhusu kuendelea kwa ujenzi wa shule ya sekondari Kibisi ambao ulikuwa umeingia kwenye mvutano baada ya kiasi cha shilingi mil 40 kilicho tengwa kwaajili ya ukamilishaji wa maboma ya shule kupelekwa…
31 October 2021, 4:10 am
Rungwe-Mbeya Ili kupunguza tatizo la udumavu na utapia mlo Jamii imetakiwa kuzingatia ulaji sahihi unaoshauriwa na wataalamu wa afya kwa watoto. Rai hiyo imetolewa na afisa lishe wilaya ya Rungwe Bi Halima Kimeta alipokuwa akizungumza na kituo hiki amesema kuwa…
28 October 2021, 5:28 am
RUNGWE katika kuendelea kuboresha huduma ya afya hapa nchini halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani mbeya inatarajia kupokea fedha kutoka serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 300 kwaajili ya ujenzi wa jengo la dhalura katika hosptali ya wilaya ya Rungwe…
27 October 2021, 5:22 am
RUNGWE. Ofisi ya mamlaka ya maji Tukuyu Wilayani Rungwe mkoani Mbeya imeahidi kutatua changamoto ya maji kwa wananchi kupitia miradi inayoenda kutekelezwa ndani ya Wilaya. Kupitia Meneja wa mamlaka ya maji Tukuyu Peter Amon amesema hayo akizungumza na Radio Chai…
26 October 2021, 9:07 am
RUNGWE Jeshi la polisi Wilayani Rungwe limewaomba wafanyabishara kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kukabiliana na watu wanao jihusisha na uwizi wa mtandaoni. Jeshi hilo limetoa kauli hiyo kupitia Mkuu wa upelezi Wilaya ya Rungwe WILLIAM NYAMAKOMANGO alipokutana na wafanyabiashara kwenye…
25 October 2021, 9:43 am
RUNGWE Mratibu wa afya ya kinywa na meno Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya DOKT HOSEA MWAKYUSA ameelezea matumizi sahihi ya miswaki ambapo mswaki unatakiwa kutumika ndani ya miezi mitatu. Akizungumza na kituo hiki amesema kuwa kinywa ni kitu muhumu katika kiungo…
25 October 2021, 9:21 am
RUNGWE Wafanya biashara wadogo (machiga) soko la Tukuyu, wamesema wameanza kutekeleza agizo la Halmashauri la kuhama katika maeneo yasiyo rasmi wanayo fanyia biashara zao na badala yake wahamie katika maeneo waliyo pangiwa na halmashauri. Wameyasema hayo wakati wakizungumza na radio…
21 October 2021, 12:09 pm
RUNGWE Vijana wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wameelezea sababu zinazo pelekea baadhi ya vijana kupata maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kutokana na tafiti zilizotolewa na tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids). Tafiti hizo za mwaka 2020 zimebainisha kuwa vijana kati…
21 October 2021, 9:33 am
RUNGWE Hivi karibuni Dunia imeadhimisha siku ya magonjwa ya afya ya akili jamii wilayani Rungwe Mkoani Mbeya ametakiwa kuachana na imani za kishirikiana juu ya ugonjwa huo. Akizungumza na kituo hiki mratibu wa afya ya akili wilaya Dkt JOHN DUNCAN…
Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.
Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.
Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.
Dira
Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora
Dhamira
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.
Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo
Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa
Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.
Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/