Chai FM
Chai FM
14 December 2021, 5:14 am
RUNGWE-MBEYA Wazazi na walezi wameaswa kuwajali na kuwathamini watu wenye uhitaji kwa kutoa mahitaji muhimu kwa watoto hao ikiwemo kuwatembelea katika maeneo mbalimbali kwani itasaidia kuongeza faraja kwao. Hayo yamezungumzwa na Umoja wa akina mama kutoka Katumba walipo watembelea watoto…
28 November 2021, 8:42 am
RUNGWE-MBEYA Mbunge wa jimbo la Rungwe ANTON MWANTONA amesema tatizo la maji linalo wakabili wanachi wa jimbo la Rungwe linaenda kumalizika baada ya serikali kutenga fedha kwajili ya kuboresha miundombinu ya maji kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungunza na na…
28 November 2021, 8:37 am
RUNGWE-MBEYA Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA ameagiza wizara ya Elimu kutenga fedha kwajili ya ukarabati wa shule zote kongwe nchini. Maagizo hayo ameyatoa wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali Mkoani Mbeya wilayani Rungwe Novemba…
23 November 2021, 9:34 am
RUNGWE Kaimu mkurugenzi kutoka mtandao wa Mashirika yanayotoa msaada wa kisheria Tanzania [TANLAP] MCHELELI MACHUMBANA ameitaka jamii kujua sheria mbambali ili kukabiliana na unyanyasaji uliopo kwenye maeneo yao. Ametoa kauli hiyo mbele ya wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani Rungwe mkoani…
22 November 2021, 9:36 am
RUNGWE-MBEYA NA:STAMILY MWAKYOMA Vijana wametakiwa kuwa vielelezo katika jamii kupitia mafunzo yanayotolewa na vyuo vya maendeleo ya wananchi hapa nchini. Kauli hiyo imetolewa na mgeni rasmi Ndugu Gerald Kimbunga katika maafali ya 45 ya chuo cha maendeleo ya Wananchi Katumba…
15 November 2021, 3:09 pm
RUNGWE-MBEYA Mwenyekiti wa chama wasioona (TLB )mkoa wa Mbeya ndg.YOHANA MONGA amewaomba wadau mbalimbali kote nchini kusaidia vifaa vya kufundishia watoto wenye mahitaji maalum mashuleni. Ametoa kauli hiyo alipokuwa akikabidhi fimbo nyeupe kwa wanafunzi wasioona kwenye shule ya mahitaji maalum…
12 November 2021, 4:59 am
RUNGWE-MBEYA Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mh,Rashidi Chuachua amewaomba wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba [mgambo]wilayani Rungwe kuenda kuyaishi yale yote waliofundishwa wakiwa mafunzoni. Ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Jeshi hilo la akiba mwaka 2021 katika halmashauri ya…
10 November 2021, 5:57 am
Jumla ya wanafunzi 4,326 wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne unaotarajiwa kuanza tarehe 15.11.2021 kote nchini. Kwa mujibu wa Afisa elimu sekondari wilayani Rungwe Mwl. Yona Mwaisaka amesema kati ya watahiniwa hao 231 ni…
9 November 2021, 6:09 pm
KYELA-MBEYA Halmashauri ya wilaya ya kyela mkoani Mbeya imeagizwa kuwafuta kazi watendaji wa kata ambao kata zao zimekuwa za mwisho kwenye zoezi la ukusanyaji wa mapato. Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera mbele ya baraza…
8 November 2021, 7:17 am
RUNGWE-MBEYA Jamii wilayani Rungwe imeendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virus vya Corona kwa kuendelea kuzingatia upataji wa chanjo inayoendelea kutolewa kote nchini. Akizungumza na Radio Chai FM Mwenyekiti wa kitongoji cha Mabonde kata ya Msasani Wilayani Rungwe Ndg.ELIAS MWASAMBILI amesema…
Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.
Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.
Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.
Dira
Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora
Dhamira
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.
Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo
Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa
Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.
Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/