Chai FM

Recent posts

14 February 2022, 12:45 pm

Uhaba wa soko kilio wakulima wa ndizi Rungwe

RUNGWE-MBEYA Kukosekana kwa soko la uhakika la ndizi imetajwa kuwa sababu inayopelekea wakulima wa zao hilo kuuza mazao yao kabla ya wakati husika. Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wakulima wilayani Rungwe  ambapo wamesema kuwa inawalazimu kuuza ndizi zao mashambani  kabla…

13 February 2022, 1:20 pm

Halmashauri ya Rungwe imekusanya mapato kwa asilimia 80%

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Rungwe limefanya kikao kilichotoa taswira hali ya ukusanyaji mapato huku Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga akiwataka Madiwani pamoja na watendaji idara mbalimbali kuendeleza juhudi za kusimamia miradi na mapato…

10 February 2022, 12:10 pm

Wauguzi wajengewa uwezo kuhusu mdomo Sungura

MBEYA Mafunzo ya siku tatu kuwajengea uwezo wauguzi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya yameanza rasmi ili kukabiliana na watoto wanaozaliwa mdomo wazi na mdomo sungura ili waweze kupatiwa matibabu mapema. Dkt Zackaria Amos ni Mkufunzi wa mafunzo hayo…

8 February 2022, 5:58 pm

Waandishi wawe chachu elimu dhidi ya vitendo vya ukatili

MBEYA Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Wilbrod Yanga amewataka Waandishi wa habari chipukizi ishirini na moja Mkoani Mbeya walionufaika na mradi wa SAUTI MPYA kuendeleza elimu waliyoipata baada ya mradi huo wa…

7 February 2022, 10:58 am

Wanafunzi waliomajumbani kwa changamoto za ujauzito warudi shule

MBEYA Serikali mkoani Mbeya kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka wanafunzi waliomajumbani kwa changamoto za ujauzito kurudi kuendelea na masomo kwa utaratibu ambao serikali imeupanga. Homera ameyasema  kuwa serikali ya awamu ya sita kupitia kwa Rais…

2 February 2022, 6:01 am

Wizi wa pikipiki wakwamisha ndoto za vijana

RUNGWE-MBEYA Wananchi wa kata ya kawetele wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa pamoja wameadhimia kuunda mpango wa pamoja wa kuanzisha ulinzi shirikishi (sungusungu) ndani ya kata hiyo kutokana na videndo vya wizi vinavyoendelea. kauli hiyo ya kuadhimia imekuja kwenye mkutano  ulioitishwa…

1 February 2022, 5:22 am

UWT Rungwe wapanda miti 50 kuendeleza uhifadhi wa Mazingira

RUNGWE-MBEYA Jumla ya miti hamsini imepandwa na Umoja wa wanawake  wa chama cha mapinduzi CCM(UWT) wilayani  Rungwe mkoani Mbeya katika Zahanati ya Suma pamoja na ofisi ya chama kwenye kata hiyo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanziswa kwa…

29 January 2022, 7:26 am

Jamii ijitokeza kupata matibabu ugonjwa wa Ukoma

RUNGWE-MBEYA Jamii imetakiwa kujitokeza kupata matibabu pindi waonapo dalili za ugonjwa wa Ukoma hali itakayosaidia kuzuia maambukizi kwa wengine. Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa kifua kikuu na Ukoma wilayani Rungwe Daktari Emmanuel Asukile alipokuwa akizungumzia kuelekea maadhimisho ya siku…

27 January 2022, 6:58 am

Abiria watoe taarifa kuepusha ajali barabarani

RUNGWE-MBEYA Tabia za kibinadamu zimepelekea kuongezeka kwa ajali barabarani kote nchini  hadi kufikia asilimia 76% kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa hivi karibuni na jeshi la polisi. Akizungumza na Radio cha FM kupitia kipindi cha Amka na Chai Mkuu wa kikosi…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/