Chai FM

Recent posts

23 February 2022, 5:21 am

Ruzuku kwa wakulima wa maparachichi itasaidia uzalishaji wa tija.

RUNGWE-MBEYA Mkuu wa walaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Dkt VICENT ANNEY ameuomba uongozi wa  chama cha ushirika UWAMARU [AMCOS] kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa maparachichi ili kuweza kuzalisha kwa tija. Ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha…

22 February 2022, 8:41 am

Ubovu wa barabara kikwazo katika maendeleo

RUNGWE -MBEYA Wafanyabiashara pamoja na wakazi wa kijiji cha Mpandapanda kilichopo kata ya Kiwira wilayani Rungwe ambapo wameeleza namna wanavyoshindwa kufanya maendeleo ya kiuchumi kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara. wakibainisha hayo baadhi ya wakazi pamoja na  wafanyabiashara wamesema…

21 February 2022, 9:45 am

Jamii yatakiwa kutowatenga wagonjwa wa fistula

RUNGWE-MBEYA NA:BETRIDA ANYEGILE Wito umetolewa kwa jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya kuachana na dhana potofu juu ya ugonjwa wa Fistula kwani ugonjwa huo unatibika bure bila mgonjwa kugharamia gharama yoyote. Akizungumza kwa njia ya Simu na Chai FM Program manager…

21 February 2022, 8:14 am

Malezi mabaya kwa watoto chanzo cha matukio ya uhalifu

RUNGWE-MBEYA Malezi mabaya kwa watoto wilayani Rungwe Mkoani Mbeya imeelezwa kuwa chanzo cha matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na mauaji. Ameyasema hayo Mch wa kanisa la Baptist Tukuyu mjini Mch. .HALLENCE MWASOMOLA, wakati akizungumza na redio chai…

20 February 2022, 5:08 pm

Wananchi wamshukuru Rais Samia fedha ujenzi shule ya sekondari

RUNGWE-MBEYA Umoja na ushirikiano  wa wakazi wa kata ya Msasani wilayani Rungwe umetajwa kuwa chanzo cha kumalizwa kwa ujenzi wa shule ya sekondari Msasani inayojengwa katika mtaa wa Bulongwe. Ameyasema hayo diwani wa kata ya msasani mh ROBIN MWAKAPESA, wakati…

16 February 2022, 10:03 am

Vijana wachangamkie mikopo ya halmashauri

RUNGWE-MBEYA. NA:JUDITH MWAKIBIBI Wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa  kujiunga na vikundi mbalimbali ilikuweza kunufaika na mikopo inayotolewa na Halmashauri ikiwa ni vikundi vya watu wenye ulemavu ,wanawake na vijana. Akizungumza na redio Chai FM ofisini kwake Mratibu Wa Dawati …

14 February 2022, 12:45 pm

Uhaba wa soko kilio wakulima wa ndizi Rungwe

RUNGWE-MBEYA Kukosekana kwa soko la uhakika la ndizi imetajwa kuwa sababu inayopelekea wakulima wa zao hilo kuuza mazao yao kabla ya wakati husika. Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wakulima wilayani Rungwe  ambapo wamesema kuwa inawalazimu kuuza ndizi zao mashambani  kabla…

13 February 2022, 1:20 pm

Halmashauri ya Rungwe imekusanya mapato kwa asilimia 80%

Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Rungwe limefanya kikao kilichotoa taswira hali ya ukusanyaji mapato huku Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga akiwataka Madiwani pamoja na watendaji idara mbalimbali kuendeleza juhudi za kusimamia miradi na mapato…

10 February 2022, 12:10 pm

Wauguzi wajengewa uwezo kuhusu mdomo Sungura

MBEYA Mafunzo ya siku tatu kuwajengea uwezo wauguzi wa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya yameanza rasmi ili kukabiliana na watoto wanaozaliwa mdomo wazi na mdomo sungura ili waweze kupatiwa matibabu mapema. Dkt Zackaria Amos ni Mkufunzi wa mafunzo hayo…

8 February 2022, 5:58 pm

Waandishi wawe chachu elimu dhidi ya vitendo vya ukatili

MBEYA Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Wilbrod Yanga amewataka Waandishi wa habari chipukizi ishirini na moja Mkoani Mbeya walionufaika na mradi wa SAUTI MPYA kuendeleza elimu waliyoipata baada ya mradi huo wa…

Kuhusu Chai FM

Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.

Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.

Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.

Dira

Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora

Dhamira

Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.

Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo

Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa

Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo

Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.

Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/