Chai FM
Chai FM
27 April 2022, 12:34 pm
Mkurugenzi wa Shule za Paradise na Patrick Mission ambaye ni mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya ,Ndele Mwaselela ameguswa kusaidia wanafunzi wenye uhitaji wapate elimu na kufungua milango ili wadau wengine waweze kujitokeza kusaidia wanafunzi wenye uhitaji . Amesema kumekuwa…
22 April 2022, 1:03 pm
RUNGWE-MBEYA Mbunge wa Jimbo la Rungwe MH. ANTON MWANTONA ametoa msaada wa vifaa kwa ajiri ya ukarabati na ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Mabonde iliyopo kata ya Msasani wilayani Rungwe. Akimwakilisha Mbunge kukabidhi vifaa katibu wa mbunge wa…
15 April 2022, 11:34 am
RUNGWE-MBEYA Mkuu wa wilaya ya Rungwe Dr.VICENT ANNEY amefanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa mapachichi kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili katika zao hilo. Wakulima zao la palachichi wa kijiji cha Ibungila kata ya Malindo wameeleza changamoto zinazowakabili katika zao…
8 April 2022, 7:43 am
RUNGWE-MBEYA Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kujua umuhimu wa fidia ya bima ya gari baada ya kupata ajali ilikuweza kupata fidia pindi apatapo matibabu. Hayo yamejiri baada ya mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Rungwe Felix Kakolanya…
3 April 2022, 6:24 am
RUNGWE-MBEYA Taasisi isiyo ya kiserikali inayotekeleza mradi wa mwanamke imara WiLDAF imetaka jamii kutoa taarifa kwenye madawati ya kijinsia pindi vitendo vya ukatili vinapojitokeza katika jamii. kauli hiyo imetolewa wana Mwanasheria SUZAN KAWANGA pamoja na mwelimishaji Ndg THOMAS MPONDA waliopokuwa…
22 March 2022, 8:47 am
RUNGWE-MBEYA Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe MPOKIGWA MWANKUGA amewataka wakulima wa zao la parachichi kuuza zao hilo kwa kufuta bei elekezi iliyotolewa na serikali ya shilingi 1600 kwa kilo. Ametoa kauli hiyo alipo kuwa akitoa elimu kwa wananchi…
18 March 2022, 9:19 am
RUNGWE Na Lennox Mwamakula Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani wilayani Rungwe mkoani Mbeya FELIX KAKOLANYA amewataka waendesha vyombo vya moto kufuata sheria za barabarani wanapo tumia vyombo hivyo. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungunza na madereva pamoja na watumiaji wengine…
16 March 2022, 11:11 am
RUNGWE, Na Sabina Martin Msaada wa mahitaji mbalimbali wenye thamani ya zaidi ya shilingi laki sita umetolewa kwa watoto yatima katika kituo cha kulelea watoto hao cha Igongwe wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake cha jicho la…
16 March 2022, 10:41 am
RUNGWE Na Lennox Mwamakula Kamati ya Bunge ya uongozi ya serikali za mitaa [TAMISEMI ] imefanya ziara wilayani Rungwe mkoani Mbeya ya ukaguzi wa barabara ya kutoka Masebe-Bugoba hadi Lutete yenye urefu wa kilometa 12 iliyo jengwa kwa kiwango cha…
9 March 2022, 10:00 am
RUNGWE-MBEYA NA:EZEKIEL KAPONELA Siku ya Mwanamke duniani leo imeadhimishwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Rungwe huku ikitolewa misaada mbalimbali kwa wahitaji. Katika maadhimisho hayo yaliyokwenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu”mamia ya wanawake…
Chai FM radio ni radio inayomilikiwa na Umoja wa wakulima wa Chai Rungwe, Ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha mkulima wa Chai wilaya ya Rungwe anapata taarifa sahihi ambazo zitasaidia kuendeleza zao la Chai pamoja na shughuli zake za kiuchumi, Elimu na Kijamii.
Uwepo wa radio Chai FM umesaidia mkulima wa zao la Chai wilaya ya Rungwe kupata taarifa kwa wakati zinazohusu zao la chai na mwenendo wake pamoja na elimu juu ya kilimo biashara kwa zao la chai na mazao mengine pamoja na ufugaji.
Hii ni kutokana na uguu wa kufikisha taarifa ya masuala ya kilimo kwa wakulima wa chai jiografia ya wilaya ikiwa ni kikwazo kwa wakulima kupata taarifa mbalimbali za ndani na nje ya wilaya pamoja na mpango wa kilimo endelevu.
Dira
Kuona jamii ya wakulima na wafugaji wa wilaya ya Rungwe wanakuwa na maisha bora
Dhamira
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya Wilaya ya Rungwe kuelimisha na kutoa taarifa za kilimo, mifugo, biashara,viwanda na habari za kijamii kupitia vipindi vya redio.
Chai Fm Radio inasikika maeneo tofauti kama ifuatavyo
Mkoa wa Mbeya – Wilaya za Rungwe, Busokelo, Kyela, na Mbeya Vijijini kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Njombe – Wilaya za Makete, Ludewa
Mkoa wa Songwe – Wilaya za Ileje na Songwe kwa baadhi ya maeneo
Mkoa wa Ruvuma – Wilaya za Mbinga na Nyasa.
Lakini pia chai Fm inapatikana ukiwa popote duniani kupitia radiotadio.co.tz/chaifm/