Jamii izingatia maziwa ya mama kwa mtoto mchanga katika kipindi cha siku 1000
31 January 2022, 5:48 am
RUNGWE-MBEYA
Wazazi wanmetakiwa kufuata utaratibu wa kunyonyesha mtoto mchanga maziwa ya mama kwa kipindi cha miezi sita kama inavyo shauriwa na wataalamu wa afya ili kumeposhia mtoto kupapa madhara ya kiafya.
kauli hiyo imetolewa na afisa lishe BI JANET MAONA kutota shirika lisilo la kiserikali litwalo I R D O alipokuwa akitoa elimu ya lishe bora kwaajia ya radio Chai Fm ambapo amesema mzazi anatakiwa kuzingatia kanuni zote za kunyonyoshesha pamoja na lishe bora kwa mtoto kwa kipindi cha siku elfu moja ambazo zitamuondolea mtoto kupata maradhi mbalimbali.
Bi MAONA mesema kuna sababubu mbalimbali zinazo pelekea mtoto kuwa na utapia mlo kuwa kuna sababu za karibu kama vile ulaji duni wa vyakula,magonjwa ya mara kwa mara,upungufu wa cha kula katika kaya
hata hivyo ameendelea kuelezea sababu inayopelekea mto kuwa na udumavu huku akitaja sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na lishe duni na kuugua mara kwa mara na kutofuata utaratibu mzuiri wa unyonyeshaji na kuto pangilia uzazi mzuri kwa baadhi ya kina mama.
sanjari na hayo Mahona amewaomba wazazi kufuata kanuni bora za unyonyeshaji na kumlisha mtoto vyakula vizuri na kufuata maelekezo wanayo pewa na wataalam wa afya