Chai FM

Mvua chanzo vifo vya watoto 15 Rungwe

27 March 2026, 3:54 pm

Uwepo wa mvua kumbwa zilizoambatana na upepo imesababisha vifo vya watu 20 huku idadi kubwa ya vifo ikiwa ni watoto.

Moja kati ya nyumba 9 zilizobomoka na kusabaabisha vifo

Na Sabina Martin

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya zimesababisha vifo vya watu 20 wengi wao wakiwa ni watoto ambao ni 15 katika kata tofauti za wilaya hii.

Hata hivyo mvua mbali na kusababisha vifo kwa wakazi hao wa Rungwe, imesababisha majeruhi ambapo baadhi ya walionusurika kuachwa bila makazi, huku baahi ya mazao ya liyokua shambani yakisombwa na maji.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh.Jaffar Hanniu  ametoa rai kwa wananchi wa Rungwe wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhama katika maeneo hayo ili kujikinga na madhara zaidi.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Rungwe

Idadi hiyo ya vifo imeongezeka kutoka vifo 18 vilivyoripotiwa hapo awali kufuatia vifo vya watu wawili katika kata ya Kinyala kitongoji cha Chunya kijiji cha Kipande.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Rungwe

Kata zilizoathirika zaidi na mvua hizi za masika ni pamoja na Kawetele, Ikuti, nkunga, lupepo na kinyala huku nyumba zaidi ya 10 zikiathirika na mvua hiyo.