Ili kukabiliana na ukataji ovyo wa miti zaidi ya kaya 500 zimepatiwa gesi Rungwe
5 September 2024, 4:45 pm
ili kuendelea kulinda misitu yetu jamii imetakiwa kupewa elimu juu ya utunzaji wa mitu ikiwa ni pamoja kutokukata miti ovyo bali ilindwe kwa kutunzwa kwa dhumini la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa mbeya kupitia chama cha demokrsia na maendeleo [CHADEMA] Sophia mwakagenda amewaomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu
Mwakagenda ametoa kauli hiyo alipokuwa akigawa mitungi ya gesi kwa wananchi wa Rungwe wakiwamo wanawake, wenyeviti wa vijiji ,watendaji wa kata na vijiji pamoja na madiwani.
Sophia nwakagenda akizungunza na wananchi wa wilaya ya Rungwe kwenye hafla ya kugaw gesi kwenye viwanja vya kivanga[Piha na Lennox Mwamakula]
sauti ya mwakagenda 1
akieleza dhumuni la ugawaji wa mitungi ya gesi amesema ni kampeni ya kupinga ukataji wa miti ovyo kwaajili ya matumizi ya mkaa.
sauti ya mwakagenda 2
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Mwenyekit wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mpokigwa Mwankuga amewaomba wanawake kuendana ili waweze kusahika nafasi mbalimbali za uongozi na wajitokeze kugombea kuanzia ngazi ya vijiji
sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe
Naye diwani wa kata ya kiwira amesema mbunge mwakagenda amekuwa mbunge wa kuigwa kwani ajabagua amewajali watuwake hivyo wananchi wandelee kumuunga mkono kwa jitihada zake za kuwatumikia wananchi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mh,Mpokigwa Mwankuga akipongeza sophia mwakaganda kwa kuwajali wakazi wa Rungwe nakuwapatia mitungi ya gesi[picha na Lennox Mwamakula]
sauti ya Diwani wa kata ya kiwira
Hata hiyo nao wananchi waliopatiwa mitungi hiyo ya gesi wamemshukuru mbunge huyo kwakuwapatia gesi hizo na wamesema wao kama wakina mama watakuwa mstari wa mbele kutoa elimu juu ya utunzaji wa miti kwadhumuni ya kunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
sauti za wananchi