Chai FM

Wakulima kunufaika na soko jipya Rungwe

11 July 2024, 8:51 am

Katibu wa mbunge jimbo la Rungwe ndg Gabriel Mwakagenda akiongea na vyombo vya habari

katika kukabiliana na changamoto ya masoko mbunge wa jimbo la Rungwe amesema kwamba serikali inatarajia kujenga soko la ndizi ili kuinua uchumi wa mkulima.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni  5.3 zimepokelelwa na halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwajili ya ujenzi ya soko la ndizi katika mji wa kiwira eneo la kalasha

kauli hiyo imetolewa na katibu wa Mbunge wa jimbo la Rungwe ndg, Gabriel Mwakagenda kwa niaba ya Mbunge wakati akiongea na vyombo vya habari kwenye eneo la mikutano Samolo Inn iliyopo mji mdogo wa katumba kwa lengo la kuelezea mafanikio yaliyopatikana na namna ya kutatua changaoto zinazo wakabili wananchi wa jimbo hilo la Rungwe

Mwakagenda amesema kwa kipindi kirefu  zao la ndizi  limekosa thamani kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika inayopelekea mkungu huuzwa kwa bei ya chini kitendo kinacho didimiza uchumi wa mkulima wa zao hilo

sauti ya katibu wa mbunge 1

Aidha Mwakagenda amezitaja fada moja kwamoja kwa moja ambazo mkulima huyo wa zao la ndizi kuwa ni pamoja na kufungua milango kwa wana Rungwe kwenda mataifa mengine kwajili ya kuuza na wananchi kuwa na uwakika wa soko sambamba na kupanda kwa thamani ya zao la ndizi

.saui ya katibu wa mbunge 2

Hata hivyo Katibu huyo amesema kutokana na historia ya wilaya ya Rungwe mazao ya kibiashara yalikuwa yakiwainiua wakulima yakuwa ni zao la chai na kahawa,hivyo kutokana kuyumba kwa soko wananchi wanalima zao jipya ambalo likuwa ni mkombozi kwao zao la parachichi ambayo inajulikana kama dhahabu ya kijani,Halmashauri ya wilaya Rungwe imepata mradi wa kujenga PARK HOUSE kwaajili ya kuhifadhia zao lisiweze kuharibika  na mkulima auze kwa tija

sauti ya katibu wa mbunge 3

Sambamba na hilo Mwakagenda ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini Mh,Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kuridhia  kutoa fedha kwaajili ya miradi hiyo kujenga soko la ndizi na park house kwajili ya zao la parachichi.