Chai FM

Halmashauri kuzuia magari kushusha na kupakia mizigo soko kuu Makambako

10 July 2024, 9:44 am

Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka katikati akizungumza na wafanyabiashara na wananchi wa Makambako hawapo pichani( Picha na Cleef Mlelwa).

Na Cleef Mlelwa – Makambako

Wafanyabiashara 112 wa mazao ambao waliingia ubia  na halmashauri ya mji wa Makambako katika ujenzi wa soko la mazao kiumba lilopo kata ya Lyamkena wametakiwa kuhamia kwenye soko hilo huku halmashauri ikikitakiwa kuzuia  magari makubwa kutoshusha wala kupakia mazao soko kuu.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka wakati akizungumza na wafanyabiashara hao katika ofisi za halmashauri ya mji wa Makambako,kutokana na zoezi la awali la halmashauri la kuwahamisha wafanyabiashara hao kukwama na kusababisha soko hilo kukosa watu,ambapo amewataka wafanyabiashara hao kuhamia katika soko hilo huku halmashauri ikitakiwa kuweka zuio la magari yenye mizigo mikubwa wa mazao kutoingia soko kuu.

Mtaka amewataka wafanyabiashara hao kuhamia katika soko hilo huku wafanyabiashara wa mazao wenye mtaji mdogo wakitakiwa kuendelea na biashara zao kwenye masoko mengine ikiwemo Soko kuu, Maguvani na Magegele.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka akitoa agizo

Aidha baadhi ya madiwani mjini Makambako, Diwani wa kata ya Mahongole Mario Kihombo na Diwani wa kata ya Lyamkena Salum Mlumbe wamesema maamuzi hayo ya mkuu wa mkoa yatakuwa na tija kwa halmashauri hasa katika kuongeza mapato.

Sauti za madiwani mbele ya wafanyabiashara na mkuu wa mkoa

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa amekubaliana na mpango huo na kueleza kuwa watasimamia maagizo hayo.

Sauti ya mwenyekiti wa halamashauri ya Makambako Hanana Mfikwa

Nao baadhi ya wafanyabiashara ambao wameingia mkataba wa ujenzi wa soko hilo na halmashauri akiwemo Mary Kyando, Abelnego Sanga na Ambwene Mbilinyi wamekubaliana na maagizo hayo huku wakikiri kupata hasara kubwa kabla ya maelekezo ya sasa.

Sauti za wafanyabiashara Makambako