Kiwango cha ufaulu chaongezeka Rungwe
3 July 2024, 6:20 pm
Ili kuwa na jamii yenye uelewa walimu wameshauriwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa lengo la kujenga kizazi chenye elimu
Rungwe-Mbeya
Na Bahati Obel
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amekemea tabia ya baadhi ya wakuu wa Shule na waalimu wakuu kudharau baadhi ya walimu kwa kufanya maamuzi wao pekeyao au na kundi lake la watu bila ya kushirikisha walimu wengine jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya taaluma katika shule .
Mkuu wa wilaya ametoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya elim katika halmashauri ya Rungwe yaliyofanyika katika ukumbi wa Landmark hotel uliopo Tukuyu ambapo amesema jambo hilo linavunja molali ya walimu na kupelekea kuto kufanya vizuri katika baadhi ya maeneo na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri pamoja na maafisa elim kuwakemea wakuu wote wa shule wenye tabia hizo.
walimu wakiwa kwenye maadhimisho ya elimu kwenye ukumbi wa landmark hotel tukuyu
sauti ya mkuu wa wilaya
Aidha Hanniu ametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi na walezi na jamii kwa ujumla kukemea vitendo vya ukatili kwa watoto vinavyo endelea kutokea nchini ikiwa ni pamoja na ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambavyo vimeanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo hapa nchini. (albino)kwa kusema kuwa vitendo hivyo havikubaliki na havitakiwi kutokea katika maeneo yetu
sauti ya mkuu wa wilaya 2
Kwa Upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe Renatusi Mchau wamesema kutokana na shule zilizopo Rungwe kufanya vizuri kumekuwepo wa uhitaji mkubwa Kwa wazazi kuwahamishia watoto wao kwenye shule za Rungwe hivyo amewapongeza walimu Kwa kutoa elimu bora Kwa wanafunzi
sauti ya mkurugenzi
Awali katika taarifa ya utekelezaji wa elimu msingi katika halmashauri ya Rungwe iliyosomwa na afisa elimu msingi Juma Mwajobe taarifa himetaja takiwimu za ufaulu Kwa kuzitaja shule 10 zilizofanya vizuri ndani ya Wilaya ya Rungwe na kubainisha changamoto zinazoikabili idara ya elimu msingi ikiwa ni pamoja na upungufu wa madarasa
sauti ya taarifa ya tathimini ya elimu
Siku ya elimu Kwa wilaya ya Rungwe imeadhimishwa Leo julai 3 mwaka 2024 yenye kauli mbiu ‘ Tumedhamiliakutoa elimu bora inayolenga kumpa maarifa,ujuzi na maadili mema ikienda sambamba na utoaji tuzo kwa wanafunzi shule na walim waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.