Chai FM

Wadau wa maendeleo kuzinufaisha shule Rungwe

3 June 2024, 3:47 pm

Mdau wa maendeleo wilayani Rungwe Ndg Aliko Mwaiteleke

Wadau wa maendeleo wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kutatua changamoto kwenye jamii

RUNGWE- MBEYA

Na Noah Kibona

Jumla ya Kompyuta 200 zinatarajia kuzinufaisha shule za sekondari 10 kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Mwaiteleke Foundation ikiwa ni hatua ya kuongeza upatikanaji wa taarifa na maarifa kwa Wanafunzi.

Kila shule itajipatia jumla ya Kompyuta Mpakato 20 zitakazosaidia kuimarisha taaluma shuleni.

Shule hizo ni pamoja na Tukuyu, Kisiba, Kinyala, Ikuti, Lupoto, Kisondela, Isongole, Nkunga, Ndembela one na Kyimo.

Aliko Mwaiteleke ni Mkurugenzi wa shirika hili ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza kuwa maabara ya kompyuta hizi itakuwa na kifaa maalumu (Server) itayaokuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu mbalimbali ikiwemo mitihani ya masomo mbalimbali ya kitaifa, kikanda na ndani ya shule.

Aidha vitabu vya masomo mbalimbali vitapatikana kupitia mfumo huu wa TEHAMA katika shule hizi na hivyo kusaidia wanafunzi kufanya rejea baada ya muda wa masomo ya kawaida.