Chai FM

Watumiaji wa soko la ndizi wanufaika Rungwe

30 May 2024, 6:37 pm

Mwakilishi wa Mwaiteleke itika nkoba akikabidhi kwaniaba vifaa kwa viongozi wa soko

kutokana na uwepo wa taarifa za magonjwa ya mlipuko jamii imeshauliwa kuchukua taadhari ili kuweza kuyaupuka

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mwamakula

Ili kukabialiana na magonjwa ya milipuko taasisi isiyo ya kiserikali ya Mwaiteleke Foundationi leo mei 30 imekabidhi vifaa vya usafi kwa viongozi wa soko la ndizi lililopo Mabonde kata ya Msasani wilayani Rungwe mkoani Mbeya

Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa wa Mbeya [UVCCM] akikabidhi vifaa kwa viongozi wa soko

Awali akizungunza kabla ya makabidhiano Mjumbe wa mkutano mkuu  mkoa [ UVCCM] Ndg Lugano  Mwambulukutu amesema mwezi uliopita waliweza kufika kwenye soko hilo na kujionea hali halisi ndiyo kiendo kilicho wasukuma na kuweza kuwatafuta wadau ili waweze kupata vifaa vya usafi kwajili ya watumiaji wa soko hilo

Sauti yaMjumbe wa mkutano mkuu  mkoa [ UVCCM

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Mwaitele Foundation Itika Nkoba aliye mwakilisha mkurugezi wa taasisi hiyo amesema walipata taarifa ya uwepo  wa changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kufanyia usafi na na kujikinga na magonjwa hivyo amefika kwaajili ya kuvikabidhi

sauti ya ITIKA

Naye Mwenyekiti wa soko hilo Amani Mwakyeja amempongeza mdau wa maendeleo Aliko Mwaiteleke kwa kuwapatia vifaa hivyo kwani vitaenda kupunguza changamoto iliyopo sokoni hpo

sauti ya mwenyekiti

Sambamba na hilo nao baadhi ya wafanyabiashara  na Mwenyekiti wa wakulima wamemshukuru Aliko Mwaiteleke kwa msaada alioutoa kwaajili ya soko hilo

sauti ya mwenyekiti na wafanyabiashara