Vitendo vya wizi vyaongezeka Rungwe
19 April 2024, 3:16 pm
Jamii imeshauriwa kutoa taarifa kwenye viongozi wa maeneo yao bindi wanapo ona vyaashiria ya uwizi au uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao.
NA lennox Mwamakula
Wananchi wa mtaa wa Mpindo uliopo kata ya Bulyaga wilayani Rungwe wamekubaliana kuanzisha ulinzi shirikishi kutokana na vitendo ya wizi vinavyoendelea mtaani hapo.
Wametoa kauli hiyo ya kuanzisha ulinzi shirikishi kwenye mkutano wa mtaa uliyo itishwa baada ya wakazi wa mtaa huo kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo nguo na kuvizitelekeza ovyo kwenye maeneo ya mtaa huo
Baadhi ya vitu vilivyo ibiwa [picha na Lennox Mwamakula]
.sauti za wananchi
Naye mmoja wa watu walio ibiwa na kunusulika kujeruhiwa baada ya kupambana na wezi hao amesema amemtambua mmoja wao kwani alimtolea kisu ili asipige kelele
sauti ya mhanga
Kwa upanda wake balozi wa mtaa huo wa mpindo Ndg Atanas kasebele amezitaja nyumba zilizo kumbwa na adha hiyo ya kuibiwa kwenye mtaa huo kuwa ni takribani nyumba tano na amesema uongozi umefika kwa kijana aliyekuwa anahisiwa ili kuweza kubaini kama kuna vitu ndani kwake vya wizi
vijana walio hudhuria kwenye mkutano wa mtaa wa mpindo [picha na Lennox Mwamakula]
sauti ya Balozi
Aidha Kasebele huyo ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa viongozi wa maeneo yao ili kuweza kuwatabua wageni wanaoingia mtaani hapo
sauti ya balozi ushauri
Sambamba na hilo mmoja wa wajumbe kwenye mkutano huo amesema kinacho pelekea vitendo vya wizi kuendelea mtaani hapo ni watu kuto hudhuria kwenye mikutano pimdi inapo hitishwa na baadhi ya wazazi kuwatetea vijana wao
sauti ya mjumbe
Hata hivyo mtendaji wa kata ya bulyaga Heriam Sambo amesema njia bekee ya kudhibiti vitendo vya wizi ni kuunda ulinzi shirikishi na kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie
sauti ya mtendaji