Mvua yasababisha majanga Rungwe
1 April 2024, 11:23 am
Moja ya nyumba iliyonusulika kubomoka [picha na Lennox Mwamakula]
Richa ya kuwepo kwa sera mipango miji nchini jamii imewaomba wasimamizi kuendelea kufuatia na kuratibu ili kufanikisha suala hilo
RUNGWE-MBEYA
Lennox Mwamakula
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameiomba serikali kuona namna kuiweka mitaa ya mji wa Tukuyu katika mpangilio mzuri ili kuondokana na ujenzi holela.
Kauli iyo imekuja kufuatia jumla ya nyumba 8 kubomoka kwa kufunikwa na udongo kutona na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kumkia siku ya jumamosi ya tarehe 23.3.2024 na kuwaacha watu hao bila makazi katika mtaa wa Bulyaga kati kata ya Bulyaga.
sauti ya wananchi
Nao baadhi ya wahanga wa tukio hilo la nyumba zao kubomolewa na mvua wameelezea namna tukilo lilivyotokea na kuiomba serikali kuwasaidia kuyaweka makazi kama yalivyokuwa hapo awali
wakazi wa bulyaga wakiwa kwenye harakati ya kufukua kifusi kwenye makazi ya watu
Sauti ya wahanga
Adam Mwaikonyole ni mwenyekiti wa mtaa huo amewashukuru wananchi wa mtaa wa Bulyaga kati Kwa ushirikiano waliouonesha Kwa kumuokoa kijana aliyekuwa amefunikwa na kifusi kwa kuondoa kifusi hicho kwenye makazi ya watu.
Wananchi wakiwa kwenye harakati ya kuondoa udongo uliyofukia moja ya nyumba[picha na Lennox Mwamakula]
.sauti ya Mwenyekiti
Aidha diwani wa kata hiyo ya Bulyaga Furaha Mwambungu amesema serikali ione namna ya kufika eneo la tukio ili iweze kufanya tathimini ya mali zilizo haribiwa na mvua hiyo na kwa kuwasaidia wahanga.
sauti ya diwani