Bei elekezi kwa zao la parachichi Busokelo
14 February 2024, 5:38 pm
Mkurugenzi wa halmashauri ya Busokelo Loema peter akisungumza kwenye kikao cha wadau wa parachichi
Wadau na wakulima wameishukuru serikali kwa kutuoa bei elekezi ya parachichi kwani itamsaidia mwananchi wa kawaida.
Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hamshauri ya Wilaya ya Busokelo Bi. Loema I Peter ameendesha kikao cha wadau wa kilimo cha zao la parachichi kilichowakutunisha wakulima wazo hilo, wanunuzi na maafisa ugani.
Kikao hicho kimefanyika leo 14/02/2024 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya Busokelo.
Akizungumza katika kikao hicho Bi.Loema amewataka wanunuzi wote waliokidhi vigezo vya ununuzi wa zao hilo kununua kwa bei ya shilingi 1,500 kwa kilo na kuzingatia matumizi sahihi ya mizani na matumizi ya stakabadhi za kielektroniki katika biashara hiyo.
Aidha Bi.Loema amewataka Wakulima wote na Wanunuzi Kuzingatia uchumaji wa Parachichi zilizokoma.
wadau wa zao la parachichi wakiwa kenye kikao
Kwa upande wake Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bi.Mwanahawa Hassan amesema kuwa kibali cha uchumaji Uchumaji na usafirishaji ndani ya halmashauri ni saa 12 jioni hadi kwenye kituo cha kukusanyia parachichi lakini ikiwa itatokea dharura wawasiliane.
Halmashauri inakusudia zao hilo linawanufaishe Wakulima wote, kikao kimeagiza kuwa malipo kwa Wakulima yafanyike kwa wakati na Kuzingatia taratibu zote za vipimo na risiti za malipo ili kuzuia utoroshwaji wa zao hilo.