Madiwani waonywa Rungwe
8 February 2024, 3:31 pm
Wanasiasa wametakiwa kuwa msitari wa mbele kuwahamasisha wananchi katika shughuli za kimaendeleo ili kuimarisha uchumi wa mmojammoja na Taifa kwa ujumla.
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu amewataka wafanyabiashara kutopanga bidhaa zao kando ya Barabara kwani kunaweza kusababisha maafa
Kauli hiyo ameitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa John Mwankenja ambapo amesma kuna baadhi ya madiwani wanatumia nyadhifa walizo nazo kuwashawishi wafanyabiashara kuuzia bidhaa zao kando ya barabara kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha maisha kwa wafanyabiashara hao.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh,Jaffar Haniu akizungunza mbele ya baraza la madiwani[picha na Lennox Mwamakula]
sauti ya mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar Hanniu
Nao baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya msasani Robin kapesa ametoa mapendekezo yake kuwa kutokana na wafanyabishara wa ndizi kwenye soko la madonde kuboreshewa miundombinu kwani katika kipindi hiki cha mvua wajengewe banda maalum ya kujifadhia sambamba na kuboreshewa eneo wanalofanyia bishara za kwani eneo hilo si rafiki.
Sauti ya diwani wa kata ya msasani
Sambamba na hilo madiwani wameshangazwa na kitendo cha zao la parachichi linalo zalishwa wilayani Rungwe kifaa cha kupima ubora wa zao hilo kwenda kupimwa hadi Makambako ambao pia nia washindani kwa kibiashara hiyo wameshauri kununuliwa kwa mashine ya kupimia zao hilo
sauti ya diwani akitoa ushauri
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Renatus Nchau amesema suala hilo ofisi yake inaendelea kufanya tafiti ya kujua mashine hiyo inauzwa kiasi gani muda wowote halmashauri itainunua ili wakulima waweze kutambua ubora unao takiwa wa wazao hilo
Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe
Mpokingwa Mwankuga ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe ameishukuru serikali ya Awamu ya sita kwa kutoa fedha kwaajili ya miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya halmashauri hiyo
Sauti ya mwenyekiti wa Halmashauri