Tahadhari yatolewa kwa wananchi wilayani Rungwe kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu
1 February 2024, 4:15 pm
Jamii imetakiwa kutunza mazingira ili kuepukana na mangojwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Na Lennox mwamakula
Wananchi wametakiwa kuchukua Tahadhari ya ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu ulioripotiwa sehemu za mikoa mbalimbali pamoja na mkoa wa jirani wa songwe.
Kauli imetolewa na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe Dokta Diocles Ngaiza alipokuwa akizungunza na chaifm ofisini kwake amesema ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa hatari hivyo kila mmoja wetu anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuweka mazingira katika hali za usafi.
Aidha Ngaiza amesema kila familia inatakiwa kutumia choo bora na kufuata kanuni za utunzaji wa choo kama unavyo elekezwa na maafisa afya waliopo kuanzia ngazi ya vijiji,kata na wilaya ili kuepukana na madhara yatokanayo na magonjwa ya mlipuko huku akiwakumbusha wakazi wa Rungwe kuwa kutakuwa na zoezi la kukagua makazi ya watu hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu asiye kuwa na choo bora.
Hata hivyo Ngaiza amesema licha ya visa vya ugonjwa huo kuripotiwa Mkoa wa jirani wa songwe ambao wakazi wake wamekuwa na mwingiliano mkubwa na wilaya ya Rungwe hivyo wanatakiwa kuchukua tahari hiyo mapema.
Sanjari na hilo Dokta Ngaiza amewaomba wananchi na viongozi wote kuendelea kushikamana ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.