Chai FM

Miaka 60 ya mapinduzi ya zanzibar yazinufaisha shule za sekondari Rungwe

13 January 2024, 5:16 pm

ikiwa dunia ikikabiliwa na mabadiliko ya tabianchi jamii imetakiwa kuwa msitari wa mbele kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi ili mvua imeze kupatikana na uzalishaji wa mazao uongezeke.

RUNGWE-MBEYA

Na Lennox Mmwamakula

Ikiwa serikali ya mapindunduzi ya Zanzibar  inadhimisha miaka 60 ya mapinduzi  mwaka huu ofisi ya mkuu wa wilaya ya Rungwe kwa kushirikiana na ofisi ya mitu ya wilaya  imeungana na watanzania wote kusherekelekea sherehe hizo kwa kupanda miti katika shule mpya ya sekondari Isaka iliyopo kata ya Nkunga wilayani Rungwe Mkoani Mbeya

Zoezi hilo la upadaji miti limeungozwa na katibu tawala wa wilaya ya Rungwe ndg,Ally Said Kiumwa ambaye alimwakilishwa mkuu wa wilaya ya Rungwe ambapo katibu tawala amesema jambo la kupandaji wa miti ni muhimu kwa kila moja wetu hivyo tuendelee kupanda miti ili kukabiliana na janga linalo ikumba ulimwengu la mabadiliko ya Tabia nchi.

katibu tawala wa Rungwe Ally Kiumwa akizungumza na wananchi wa kata ya nkunga wakati wa upandaji wa miti [picha na Lennox Mwamakula]

Akisoma Taarifa mbele ya mgeni Rasmi afisa maliasili wa wilaya ya Rungwe Numwagale Bugali amesema Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imejiwekea malengo ya kupanda miti milioni moja na laki tano kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

sauti ya afisa misitu 1

Hata hivyo  Bugali amesema katika halmashauri ya Rungwe kuna wadau mbalimbali ambao wanashirikana nao ambao wanapatikana kwenye kata mbalimbali na inasaidia jamii kupata miti ya kupanda kwenye maeneo yao

afisa mitu Numwagile bugali akisoma taarifa mbele ya katibu tawala wa wilaya ya Rungwe

sauti ya afisa misitu 2

Aakijibu taarifa hiyo katibu tawala wa wilaya ya Rungwe amesema lengo la serikali ni kuendeleza utunzaji wa misitu kwenye maeneo yetu hivyo ametoa rai kwa walimu wa shule ya sekondari isaka kutunza miti iliyo pandwa shuleni hapo

katibu tawala akipanda mti kwenye shule ya sekondari isaka

sauti ya katibu tawala 1

Aidha Kiumwa amesema jamii isishie kupanda miti ya kivuli pia miti ya matunda mbalimbali inahitajika kwani itasaidia wanafunzi kupata matunda wakati wawapo shuleni hapo

sauti ya katibu tawala 2