Wakazi Kisondela Rungwe wapeleka kilio cha maji kwa spika wa bunge
4 January 2024, 7:45 pm
Suala la maji limekuwa changamoto kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe licha ya kuwepo kwa vyanzo vingi vya maji ndani ya wilaya hiyo.
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
wananchi wa Kijiji cha Kibatata Kata ya Kisondola Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wamefikisha kilio cha maji mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia alipofanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo.
wamesema changamoto kubwa wanayo kabiliana nayo wananchi tangu kuzaliwa kwao hajawai kuyaona maji safi na salama kitendo kinacho wapelekekea kutumia maji ya mito
sauti za wanachi wakilia juu ya maji
Kilio hicho kinaungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Sophia Mwakagenda kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo [CHADEMA] amesema kilio cha kazi hao kinatakiwa kufunyiwa kazi
Mh, spika wa Bunge la jamhuri ya Tanzania Tulia Ackson akizungumza na wakazi wa kata ya kisondela
sauti ya mwakagenda
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mpokigwa Mwankuga amesema serikali inatekeleza miradi mbalimbali ukiwemo wa kata ya kisondela ambapo amesema utakapo kamili utaondoa kilio cha wananchi wa Kisondela na maeneo ya jirani
sauti ya mwenyekiti wa halmashauri
Naye Mtendaji Kata ya Kisondela Lusajo Kibona ametoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji ameioma serikali kukamilisha mradi huo kwa haraka ili wanachi waondokane na changamoto ya maji
sauti ya mtendaji wa kata
Kwa upande wake Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson amesema kilio hicho amekichukua kwa uzito mkubwa kinaenda kufanyiwa kazi
sauti ya spika wa Bunge la Tanzania
Naye Naibu Waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewatoa hofu wananchi wa Kyela na Rungwe kwa serikali inaendelea na mkakati wa kulitumia Ziwa Nyasa kama chanzo kikubwa cha maji
Sauti ya Naibu waziri wa maji
Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mikubwa na midogo ikiwemo ya uchimbaji wa visima ambapo kila mkoa umepatiwa gari la kuchimba visima.