Wadau wa maendeleo wazidi kuing’arisha Rungwe
31 December 2023, 8:34 pm
Katika kuhakikisha ofisi Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa na mwonekano mzuri wadau mbalimbali wameendelea kujitokeza kukarabati majengo ya chama hicho wilayani Rungwe.
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Mkurugenzi wa Taasisi ya mwaiteleke Foundation Aliko Mwaiteleke amewaomba wadau mbalimbali wa maendeleo nchini wakiwemo wazawa wa Rungwe kujitokeza kusaidia kuijenga wilaya ya Rungwe ili kuendelea kuutunza mji kongwe wa kistoria hapa nchini
Jengo la ofisi ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Ibighi
Ametoa kauli hiyo kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi kata ya Ibighi alipokuwa akikabidhi tofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama hicho kutokana na jengo la awali kuchakaa, hivyo Mwaiteleke amesema kama chama ndicho kimeshika madaraka hivyo wadau wa maendeleo watakuwa bega kwa bega kuboresha mazingira ya chama ikiwa ni pamoja na miundombinu ya ofisi za chama kuanzia ngazi ya vijiji, kata hadi wilaya.
Sauti ya mwaiteleke
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya ibighi Itika Nkoba mwakatwila ameipongeza Taasisi ya Mwaiteleke foundation amesema kutokana na harambee iliyofanyika kwenye viwanja vya chama hicho baada ya kualika wadau mbalimbali na kuchangia kwajili ya ujenzi hivyo amesema kwaniaba ya chama wamepokea tofari na wananshukuru mkurugenzi wa taasisi hiyo kwa kusaidia ujenzi wa ofisi hiyo ya chama
mkurugezi wa mwaiteleke foundation akimkabidhi mwenyekiti wa chama tofari kwajili ya ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi [picha na Lennox mwamakula]
sauti ya mwenyekit wa chama kata ya ibighi
Naye katibu wa chama cha mapinduzi kata ya ibighi Twalib Mwaijumba pamoja Amida Sanga ambaye ni mjumbe wa halmashauri ya kata wamesema tangu ujenzi waofisi uwanzishwe Aliko Mwaiteleke amekuwa msaada mkubwa kukakikisha ofisi hiyo inakamilika
sauti ya katibu wa chama na mjumbe