Wadau wa maendeleo wasaidia ujenzi wa madarasa Rungwe
29 December 2023, 10:32 am
ikiwa shule zinatarajiwa kufunguliwa wadau wa maendeleo nchini wameomba kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha miundombinu ya shule
Mkurungenzi wa Mwaiteleke foundation [kulia]akizungumza baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi[picha na Lennox mwamakula]
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox mwamakula
Ili kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari kibisi mkurugenzi wa taasisi ya Mwaiteleke Foundation Aliko Mwaiteleke amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili.
Akikabidhi vifaa hivyo mkurugenzi wa taasisi hiyo Aliko Mwaiteleke amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo kuwa kuna changamoto ya kuhamirishaji wa madarasa mawili shuleni hapo wao kama wadau wa maendeleo wameona haja ya kuiunga mkono serikali lli ifikapo mwezi wa kwanza watoto waweze kuaza masomo yao bila kiwazo
Mwalimu shule ya sekondari kibisi akipokea computer mpakato kutoka kwa mkurugenzi wa Mwaiteleke Foundation
Mkurugenzi wa taasisi hiyo ametaja vifaa vilivyo kabidhiwa shuleni hapo kuwa ni mbao kwaajili ya kupaulia ,saruji pamoja na computer mpakato kwajili ya kutunzia kumbumbu za shule na mambo mengine yanayo hitaji computer.
sauti ya aliko mwaiteke
Kupande wake Diwani wa kata ya kyimo Basic kasote amemshukuru mkurungenzi wa Taasisi ya Mwaiteleke kwa kuwaunga mkono kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo ya sekondari na amemuomba kuwa kutokana na shule hiyo kuwa mpya bado kuna mahitaji mengi kama vile shule haina hostel,maabara uzio hivyo aendelee kuikumbuka shule ya sekondari kibisi
sauti ya diwani kata ya kyimo
Naye mkuu wa shule ya sekondari kibisi ameishukuru taasisi hiyo ya mwaiteleke foundation kwa kusaidia ujenzi pamoja na kuwapatia computer amesema itakwenda kuraisisha utendaji wao wa kazi shuleni hapo
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa shule ya sekondari kibisi[picha na Lennox mwamakula]
sauti ya mwalimu
Sambamba na hilo naye mtendaji wa kata ya kyimo Ndinagwe Mwakigonja kwa niaba ya wananchi wa kibisi wamemshukuru Aliko Mwaiteleke kwakuwapatia saruji pamoja na mbao kwani kwao ilikuwa changamoto kubwa ya namna ya kuwapokea wanafunzi pindi shule zitakapo funguliwa January 8 mwakani
sauti ya mtendaji