Tulia asambaza ujumbe wa upendo kwenye jamii
17 December 2023, 10:59 am
katika kuhakikisha jamii inakuwa na usawa Taasisi ya Tulia Trust imeendelea kukipinda bendera ya yenye ujumbe wa upendo na kwa kuwatembelea watu wenye mahitaji mbalimbali wirayani Rungwe.
Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Ttrust Joshua Mwakanolo akiwa na vijana pamoja na viongozi wengine katika harakati ya kukimbiza bendela
RUNGWE-MEYA
Na Lennox Mwamakula
Taasisi ya Tulia Trust imekamilisha ziara ya siku 7 ya kukimbiza bendera ya Upendo iliyobeba ujumbe wa upendo, mshikamano na uwajibikaji ambapo leo imefika katika hospitali ya wilaya Tukuyu na kukabidhi vitu mbalimbali kwaajili ya wagonjwa kwenye wadi la watoto.
Akikabidhi msaada huo Afisa Habari wa Taasisi hiyo Joshua Mwakanolo amesema wametembelea Hospital hiyo kutokana na hospital hiyo kuwa na wagongwa wengi kutoka maeneo mbalimbali ili kuweza kuwatia moyo.
Pia taasisi hiyo wamefanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo kwa lengo la kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Sauti ya joshua
Awali taasisi ya Tulia Trust wamewatembelea wahitaji akiwemo Elias Mwakalundwa mwenye changamoto ya ulemavu wa miguu na mikono ambapo wamemkabidhi kitimwendo kitakachomsaidia kufika maeneo mbalimbali ambayo hapo awali alikuwa akishundwa kufika.
Afisa habari wa Trust Joshua mwakanolo akikabidhi kitimewndo mmoja wa uitaji Ndugu Elias mkazi wa kata ya makanandana
Pia wameahidi kutoa magongo kwaajili ya kumsaidia Mwananchi wa kijiji cha ndembela kata ya makandana kwajili ya kumsaidia kutembea kutokana na changamoto ya kiafya inayomkabili.
sauti ya Joshua
Kwa upande wake diwani wa kata ya Makandana Boniface Mwasikili amewashukuru Taasisi ya Tulia Trust pamoja na Mkurugenzi wa taasisi hiyo spika wa bunge na mbunge wa Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson kwa kufika na kutoa msaada kwa wahitaji ndani ya kata hiyo.
Joshua Mwakanolo akikabidhi baadhi ya vitu alipotembela wadi la watoto katika hospitali ya Makandana
sauti ya Diwani
Taasisi ya Tulia Trust inakimbiza bendera ya upendo inayoambatana na ujumbe wa Upendo, Mshikamano na uwajibikaji na kuwafikia wahitaji mbalimbali ndani ya halmashauri ya wilaya ya Rungwe, ambapo pia afisa habari wa taasisi hiyo ametoa rai kwa watanzania kudumisha upendo na mshikamano
Afisa habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo akiwa na viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Rungwe katika ofisi za chama hicho
sauti joshua mwakanolo