Wanawake wilayani wakomesha ukatili
9 December 2023, 5:07 pm
kufuatia na kuwepo kwa vitendo vya ukatili kwenye jamii wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuripoti kwenye vyombo vya sheria.
RUNGWE-MBEYA
Na Lethicia Shimbi
Ikiwa bado ni Mwendelezo wa kampeni za kupinga ukatili wa kinjinsia Duniani Wanawake Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wametakiwa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia pindi tendewa majumbani kwao.
Hayo ameongea Lusajo Fred Kibonde Kaimu Mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake Wilaya ya Rungwe wakati wa akikabidhi vifaa kwa wanawake waliojifungua katika hospitali ya wilaya Rungwe[ Makandana] amesema kuwa mwanamke yeyote atakaye fanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia ni vyema akafika kwenye dawati la jinsia ili kutoa taarifa.
sauti ya kaimu mwenyekiti Lusajo kibonde
kaimu mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake akikabidhi moja ya bidhaa kwenye hospitali ya wilaya[picha na lethicia shimbi]
Lusajo Kibonde amesema kuwa kupitia mtandao wa polisi wanawake wilaya ya Rungwe wameamua kufika hospitalini hapo kwa lengo la kutoa elimu na kukabidhi vifaa hivyo kama vile sabuni , sukari,pamoja na pampasi za watoto kwa mama aliyetoka kujifungua kwani wanawake wamekuwa walengwa wakubwa wa kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
sauti ya kaimu mwenyekiti
Naye Bupe Sucka kitengo cha Dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi Wilayani hapa amewaomba wanawake kuwa karibu na watoto wao ili waweze kubaini vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na kuweza kutoa taarifa kwenye dawati la jinsia .
sauti ya Bube sacka
Kwa upande wake Nesi wa Hospitali ya Wilaya ameshukuru kitendo kilichofanywa na mtandao wa polisi mwanamke Wilaya ya Rungwe kwa kuwafikia wanawake na kuwapatia mahitaji hayo na amewashauri wanawake wote kutokuwa na miyo ya kukata tama pindi wanapokutana na vitendi vya ukatili wa kijinsia
baadhi ya vitu vikikabidhiwa na wanawake wa dawati la mtandao la jeshi la polisi wilayani Rungwe[picha na lethicia shimbi]
sauti ya nurse wa hospitali ya wilaya
Sanjali na hayo baadhi ya wanawake waliyotembelewa na kupatiwa mahitaji hayo wametoa shukurani na kuwataka waendelee na moyo huo wa utoaji.
mmoja ya wanawake waliotembelewa hositalini hapo akikabidhiwa moja ya zawadi kwenye wodi la wazazi
sauti ya wanufaika
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huanza kila ifikapo novemba 25 na kufikia kilele decemba 10 ya kila mwaka ikiwa na lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili kwa jamii huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia”.