Polisi kukabiliana na vitendo vya kikatili Rungwe
29 November 2023, 8:54 am
ili kuweza kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ukatili kwa wanawake na watoto jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa kwenye vyombo vya kisheria.
RUNGWE-MBEYA
Na Lennox Mwamakula
Jamii imeshauriwa kuachana na vitendo vyaa kikatili vinavyo sababisha vifo na kupelekea kuacha familia hasa watoto kuishi kwenye mazingira magumu
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa usalama Barabarani kutoa jeshi la polisi wilayani Rungwe Felix Kakolanya kwenye mkutano wa hadhara uliyo fanyika kjiji cha kawetele chini kata ya kawetele wilayani Rungwe ambapo amesema kuna madhara makubwa kwa mzazi anaye fanyiwa pamoja na mtoto ikiwa ni kuthirika kiakili.
sauti ya kakolanya o1
Aidha Kakolanya amesema kumekuwepo na vifo vingi wilayani Rungwe kutokana na baaadhi ya watumiaji wa Barabara hasa watembea kwa miguu kutofuata sheria zilizopo na wengine kuvuka Barabara wakiwa wamelewa kitendo kinacho changia mtu kugongwa na kupotenza uhai.
Mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani wilayani Rungwe Felix Kakolanya [Picha na Lennox Mwamakula]
Hivyo amewaomba wananchi kwa kipindi hiki cha mwisho mwa mwaka kutumia barabara vizuri na amesema wauzaji wa pombe za kienyeji wafuate muda ulipangwa wa kufungua biashara zao kwani operesheni maalum ya kuwachukulia hatua za kisheria inaanza
sauti ya kakolanya o2
Kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi Tukuyu Asp Raphael Mlangwa amesema watoto wanafanyiwa vitendo mbalimbali vya kikatili likiwemo suala ulawiti kwa watoto kushamili hivyo amewasihi wazazi na walezi kuwa karibu watoto ili kukabiliana na vitendo vya ukatili vilivyopo ndani ya jamii.
sauti ya mkuu wa kituo
Naye mwenyekiti wa kijiji cha kawetele chini Alphonce Mwabulambo amewaomba wakazi wa kawetele kutoa taarifa ya vitendo vya kiharifu Kama vile uwizi wa kuku,Bata na Nguruwe vinavyo endelea kijijini hapo ili wahusika wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria
Mkuu wa kituo cha polisi Tukuyu ASP Raphael Mlangwa [picha na Lennox Mwamakula]
sauti ya mwenyekiti
Sambamba na hilo jeshi la polisi wilayani Rungwe wananchi kugombaniana ardhi kwani kumekuwepo na kesi nyingi za migogoro ya ardhi vitendo kinacho pelekea kuuana na kutoelewana kwenye famila na jamii kwa ujmla
sauti ya jeshi la polisi