Bei elekezi ya parachichi iliyotolewa na serikali yawanufaisha wakulima Rungwe
23 November 2023, 3:53 pm
Kutokana na kuwepo kwa wanunuzi wanaowadanganya wakulima, serikali imeamua kutoa bei inayotakiwa kampuni zinunue parachichi ili kumkomboa mkulima.
Mkuu wa mkoa akizungumza na wadau wa parachichi[picha na Lennox Mwamakula]
Afisa kilimo wa wilaya Juma Mzala amebainisha utaratibu wakufuata kwa mnunuzi wa zao hilo kuwa kila mnunuzi anatakiwa kutuma maombi yakupata kibari cha ununuzi wa parachichi kwa katibu mkuu wa wizara ya kilimo pamoja na leseni ya biashara ili aweze kutambulika kwenye wilaya husika
Afisa kilimo wa wilaya akiwasilisha mpango mkakati wa wilaya mbele ya mkuu wa mkoa
Baada ya kusomwa kwa muongozo nao wakulima wazao hilo wamewasilisha vilio vyao ikiwemo suala la ninani anatakiwa kuchuma parachichi likiwa shambani kutokana na wanunuzi kutelekeza parachichi baada ya kuchumwa kwa madai kuwa halijakidhi viwango.
sauti ya mkulima
Kwa upande wake mkuu wa mkoa amesema mnunuzi ndiye anayetakiwa kuchuma parachichi ilikuondoa mkanganyiko uliopo kwani mkulima hana elimu juu ya parachichi la kiwango kipi ambalo mnunuzi ana lihitaji hivyo akichuma parachichi anatakiwa alilipie mwenyewe.Hata hivyo katika kikao hicho cha wadau waparachichi hasa makampuni wamekubaliana kuchangiakiasi cha fedha kwajili ya maendeleo ndani ya wilaya ikiwemo afya, elimu na maji
sauti ya mkuu wa mkoa 02