Michango ya chakula mashuleni kuchochea ufaulu Rungwe
20 November 2023, 4:10 pm
uwepo wa chakula mashuleni kunasaidia kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi pia kuna mjengea uwezo wa uwelewa
RUNGWE -MBEYA
Na Lennox mwamakula
Mkuu wa shule ya msingi Mabonde iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya Christine Ndimbo amewaomba wazazi na walezi kujenga utamadudu wa kuhudhuria vikao vya wazazi vinavyo hitishwa mashuleni.
Ametoa kauli ameitoa alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Amka na chai ambapo amesema ameshangazwa na taarifa za kuwepo kwa michango mingi kwenye shule yake amesema habari hizo hazina ukweli kwani michango inayo changishwa ni ile ambayo wazazi walikubaliana kwenye vikao vyao ukiwemo mchango wa chakula
sauti ya mkuu wa shule 1
Hata hivyo amesema mnamo tarehe 8 mwezi wa Tano Mwaka huu, wazazi waliadhimia kuwepo kwa mchango wa kutoa mazao kama mahindi,fedha kwaajili ya mlinzi pamoja na kiasi cha fedha ili kununulia kuni kuwepushia usumbuffu mwanafunzi kutoka na kuni nyumbaniAidha amesema walimu wamepewa miongozo inayo tolewa na wizara ya elimu inayo utaratibu wa kufuata hivyo hawawezi kuenda kinyume na utaratibu wa serikali
sauti ya mkuu wa shule 2
Sambamba na hilo amewaomba wazazi/walezi na jamii kwa ujumla kuwa kama kuna suala limejadiliwa kwenye vikao vya wazazi kila mmoja anatakiwa kueshimu maamuzi yaliyo amulilwa kwenye kikao husika cha wazazi katika shule husika