Siku 16 za kupinga ukatili; “wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia”
20 November 2023, 12:51 pm
Na Sabina Martin: Rungwe- Mbeya
Kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya imetakiwa kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili vinavyoendelea katika maeneo yao ili kutokomeza vitendo hivyo.
Akizungumza katika kipindi cha amka na chai Bw. Eddie Mwangalaba ambaye ni msaidizi wa kisheria kutoka wilaya ya Rungwe inakabiliwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa kimwili, ukatili wa kihisia pamojana ukatili wa kiuchumi.
Akifafanua zaidi kuhusu ukatili wa kiuchumi Mwangalaba amesema kuwa baadhi ya wananchi wanaelewa kuhusu ukatili wa kiuchumi ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Katika hatua nyingine ametoa rai kwa jamii kuacha kuwatumia wanasiasa kwenye mashauri ya kisheria badala yake wawatumie wasaidizi wa kisheria ili kupatiwa elimu zaidi.
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huanza kila ifikapo novemba 25 na kufikia kilele decemba 10 ya kila mwaka ikiwa na lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili kwa jamii huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “wekeza kuzuia ukatili wa kijinsia”.