Familia ya Mwansasu yawashukuru watanzania
13 November 2023, 3:27 pm
Jamii imeshauriwa kuwaombea viongozi wa serikali ili waweze kuwatumikia kwa moyo
Mh,Tulia akiwashukuru wana Rungwe kwa kumuombea kwenye shuguli za Serikali [picha na lennox mwamakula]
RUNGWE.MBEYA
Na Lennox mwamakula
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amewaomba watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kuwaombea viongozi wao wa serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia.
Kauli hiyo ameitoa kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na familia ya Ackson Mwansasu ya kuwashukuru wana Rungwe kwa kumwombea mtoto wao baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa mabunge duniani [IPU] iliyofanyika nyumbani kwao kijiji cha Mpindo kata ya Bulyaga wilayani Rungwe.
Akisoma taarifa ya kushukuru mmoja wa wana familia amesema lengo ya kuandaa hafla hiyo ni kumtolea Mungu sadaka ya shukrani kwa kumwezesha Dkt. Tulia kupata nafasi hiyo ya kuwa raisi wa mabunge duniani kwani Mungu pekee ndiye aliyetoa kibali hicho.
sauti ya familia wakati wa kusoma taarifa fupi
Wakazi wa wilaya ya Rungwe wakiwa kwenye hafla ya maombi nyumbani kwao spika Tulia [picha na lennox Mwamakula]
Kwa upande wao machifu wilayani Rungwe wakiongozwa na chifu JOEL MWAKATUMBULA wamesema wanaendelea kumuombea kwa Mungu dkt Tulia kwani ameishimisha wilaya ya Rungwe,Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla si kwa matakwa ya wana Rungwe bali ni mapenzi ya Mungu.
Sauti ya chifu wa wilaya ya Rungwe,chifu Mwakatumbula
Nao baadhi ya wabunge walio hudhuria hafla hiyo akiwemo mbunge wa jimbo la Makete Festo Sanga na jimbo la mbarali Bahati ndingo wamesema kuchanguliwa kwa mh, Tulia kuwa Rais wa mabunge duniani watanzania wamuombe kwa mungu ili atimize majukumu yake vizuri kusiwe na mtu wa kumkwamisha.
Mbunge wa jimbo la Makete Mh,Festo Richard Sanga akiongea na waandishi wa habari[picha na lennox Mwamakula]
Sauti za wabunge kwenye hafla ya kumuombea Dr Tulia
Aidha mku wa wilaya ya Rungwe Jaffar Haniu amesema serikali ya wilaya itaendelea kumpa ushirikia kwa kila hatua atakayo ifanya ya kutekeleza majukumu yake ya kila siku katika kulitumikia taifa na dunia kwa ujumla.
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Rungwe
Hata hiyo kwa upande wake DR TULIA amesema watanzania waendele kumuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Dr Samia Suluhu Hasan kutokana na jitihada zake za kuwatumikia wananchi
Sauti ya Mh,tulia