Ujio wa vituo vya afya kuwa mkombozi kwa wananchi
7 October 2023, 8:11 am
kituo cha afya ndanto {picha na lennox mwamakula}
wananchi wafurahia huduma ya afya wilaya rungwe kutokana na kuondokana na changamoto ya muda mrefu.
RUNGWE-MBEYA
Na lennox mwamakula
Jumla ya wakazi elfu kumi na nanene wanaenda kunufaika na huduma ya afya pindi ujenzi wa jingo la mama na mtoto litakapo kamilika kwenye kituo cha afya kata ya ndanto utakapo kamilika
Samwel Mwinuka ni diwani wa kata ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na mwanahabari wetu alipotembelea kata hiyo na kujionea shughuli za maendeleo hasa ujenzi wa kituo cha afya kilichojengwa kijiji cha cha Ntokela.
Amesema uwepo wa kituo cha afya ndani ya kata hiyo kumesaidia kuondolea adha ya kutembea umbali mrefu ya kufuata huduma hiyo kwani awali wananchi walikuwa wakifuata huduma hiyo katka hospitali ya mission igogwe na hosptali ya wilaya Makandana
Sauti ya mwinuka 1
Aidha mwinuka amewaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kujitoa kwenye shughuli za maendeleo kwani bado changamoto bado zipo kama vile uboreshwaji wa miundombinu ya barabara,kwani serikali ni sikivu suala la Barabara utafanyika kadili fedha zitakapo patikana
SAUTI YA MWINUKA 2
Kwa upande wake Sara osiah mkazi wa kata hiyo imeshukuru serikali kwa kuwasogezea huduma ya afya kwani amesema kumewasaidia kuondokana na adha ya kufuata huduma hiyo kwenye kata za jirani ambapo huduma zilikuwa zikipatikana
Sauti ya sara