Mwenge wa uhuru kukimbizwa kilomita 156 Rungwe.
6 September 2023, 11:08 am
RUNGWE – Mbeya
Wananchi wilayani Rungwe watakiwa kuchangamkia fursa ya uwepo wa mbio za mwenge kuongeza kipato chao.
Na Lennox Mwamakula
Wananchi Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya Wametakiwa Kujitokeza Kwa Wingi Wakati Mapokezi Ya Mwenge Wa Huru Katika Kijiji Cha Ikuti Septemba 7 Mwaka Huu .
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Rungwe Jaffar Hanniu Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ofisini Kwake Amesema Halmashauri Ya Wilaya Ya Rungwe Imepewa Heshima Kuupokea Mwenge Wa Uhuru Kimkoa Ukitokea Katika Mkoa Wa Songwe.
Sauti ya DC 1…………….
Hanniu amesema Kuwa Mwenge Wa Uhuru Utakimbizwa Kwa Umbali Wa Kilomita 156 huku ukitarajiwa kuzindua Miradi Na Kuweka Jiwe La Msingi Katika kata za Ikuti , Malindo Katika Kijiji Cha Kapughi , Kijiji Cha Makandana Katika Hospitali Ya Makandana , Bulyaga , Shule Ya Sekondari Tukuyu , Msasani ,Bagamoyo , Ibigi , Kyimo Pamoja Na Kiwira.
Sauti ya DC 2……………..
Aidha Amesema Katika Siku Hiyo Ya Tarehe Saba Kutakuwa Na Mkesha Pamoja Na Burudani Hivyo Amewataka Wananchi Wajitokeze Kwa Wingi Wakati Wa Kupokea Mwenge Pamoja Na Kukagua Miradi.
Sauti ya DC 3……………
Hata hivyo Amesema Mwenge Wa Uhuru Utakabidhiwa Katika Halmashauri Ya Kyela Tarehe 8 Katika Eneo La Machimbo La Makaa Ya Mawe Kiwira Mwenge Wa Uhuru Utakabidhiwa Katika Halmashauri Ya Kyela .
Sauti ya DC 4………