uhaba wa chakula shuleni chanzo cha matokeo mabaya Busokelo
8 May 2023, 8:22 am
RUNGWE
Na, Robert Mwakyusa
Walimu wilayani Rungwe wameaswa kuwa na mbinu mpya za ufundishaji ili kuboresha ufaulu wa wanafunzi wa masomo ya sayansi.
Hayo yamejili kwenye baraza la madiwani lililo fanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa halmashuari ya Busokelo.
Aidha mwenyekiti wa halmshauri hiyo mh.Njobero amesema matokeo ya kidato cha pili kwa masomo ya physics na mathermatis ni mabaya hivyo yanahitaji nguvu ya ziada.
Wakizungumza katika baraza hilo madiwani wameainisha sababu za kufeli kwa wanafunzi ikiwemo ukosefu wa chakula shuleni,uhaba wa walimu,walimu kuwa na majukumu mengi yanayo pelekea kukosa mda wa kuwa karibu na wanafunzi.
Katika kutatua hilo baraza limekubaliana kuongeza idadi ya walimu wa sayansi walio hitimu vyuo vikuu ,kuhimiza wazazi kutoa michango ya chakula , na walimu kutimiza majumu yao ipasavyo.
Hata hivyo Katibu tawala wilaya ya Rungwe Bw. Nkondo Bendera akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya amewataka viongozi wa idara na viongozi wa chama kufanya ziara ya mara kwa mara shuleni na walimu kutumia mbinu sahihi za kufundishia.