wakulima wilayani Rungwe wametakiwa kutumia mbolea kwa usahihi
12 October 2022, 3:56 pm
RUNGWE-MBEYA
NA:SABINA MARTIN
Kuelekea madhimisho ya siku ya mbolea duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo octoba 13 wakulima wilayani hapa wametakiwa kutumia mbolea kwa usahihi ili kupata mazao mengi.
Akizungumza kwa njia ya simu na Chai FM afisa kilimo wilayani hapa Bw. Juma Mzara amesema kamba kuna dhana ya baadhi ya wakulima kuchanganya mbolea tofauti tofauti bila utaalamu hali inayopelekea wakulima wengi kutumia gharama kubwa bila kupata faida.
Aidha amesema wilaya imekuwa na shughuli ya kutoa elimu katika maeneo mbalimbali kwa wakulima kuanzia ngazi ya kata.
Kuhusu mbolea za ruzuku Mzara ametoa rai kwa wakulima kuendelea kujiandikisha ili kupata mbolea hiyo, huku akisisitiza wakulima kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea hizo.
Siku ya mbolea duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Oktoba ikiwa ni kumbukizi ya uvumbuzi wa kirutubishi aina ya Amonia kinachopatikana hewani uliofanywa na mwana sayansi kutoka nchini Uingereza Fritz Haber mwaka 1908, na iliadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani tarehe 13 Oktoba 2016 nchini Uingereza kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu faida na matumizi sahihi ya mbolea.
Maadhimisho hayo ya mbolea mwaka huu 2022 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo ajenda ya 10/30, matumizi sahihi ya mbolea ya ruzuku kwa kilimo chenye tija.