Jamii imetakiwa kusalimisha silaha haramu
23 September 2022, 5:41 am
RUNGWE-MBEYA
NA,JUDITH MWAKIBIBI
Kutokana na kampeni inayoendelea ya usalimishaji wa silaha kitaifa wananchi wilayani Rungwe mkoani Mbeya wametakiwa kusalimisha silaha haramu zinazomilikiwa kinyume na utaratibu.
Akizungumza katika studio za radio chai FM mrakibu wa jeshi la polisi Wilayanl ya Rungwe Sevelini Msonda amesema kuwa kila ifikapo mwezi wa tisa kunakuwa na kampeni kitaifa ya kusalimisha silaha haramu .
Aidha amesema Jeshi la Polisi Wilaya ya Rungwe limejipanga vizuri na kuhakikisha zoezi linafanyika kikamilifu na pindi kampeni ikikamilika utaanza msako kubaini wanaomiliki silaha kinyume na sheria.
Hata hivyo mrakibu wa jeshi la polisi amesema mpaka sasa kwa wilaya ya Rungwe hamna mwananchi yeyote aliyesalimisha silaha hivyo ni vyema mwananchi anayemiliki silaha kinyume na utaratibu wa kisheria ajitokeze.