Jamii iwapeleke watoto wapate chanjo ya polio
10 September 2022, 7:47 am
RUNGWE-MBEYA
NA:WANDE BUSHU
Mratibu Wa Chanjo Katika Halmashauri Ya Wilaya Rungwe Mkoani Mbeya Ezekiel Mvile Amewaomba Wazazi Kuwapeleka Watoto Wao Katika Vituo Vya Afya Waweze Kukamilisha Dozi Ya Polio ili Iweze Kuwakinga Na Ugonjwa Huo.
Ameyasema Hayo Wakati Akizungumza Na Chai Fm Huku Akieleza Kuwa Kundi Kubwa Linaloathirika Na Ugonjwa huo Ni Watoto Walio Chini Ya Umri Wa Miaka Sifuri Hadi Miaka Kumi Na Tano.
Aidha Mvile Ameongeza Kuwa Kwa Mujibu Wa Utaratibu Wa Serikali Watoto Chini Ya Umri Wa Miaka Mitano Ndio Wanatakiwa Kupata Chanjo Ya Polio Na Endapo Mtoto Amepata Chanjo Awali Na amevuka Umri Wa Miaka Mitano Anatakiwa Amalizie Dozi Hizo Kwani Hazina Madhara
Pia Mvile Amehitimisha Kwa Kusema Kuwa Mtoto Ili Awe Amekingwa Kikamilifu Na Ugonjwa Huo Anatakiwa Apate Dozi Nne Za Chanjo Ya Polio.
Kwa Upande Wao Wananchi Wa Wilaya Ya Rungwe Wamesema Hawana Uelewa Wowote Kuhusiana Na Ugonjwa Huo Hivyo Wamewaomba Wataalamu wa afya Kuwapatia Elimu Juu Ya Ugonjwa Huo.